Raga

Kenya yapagwa na New Zealand michezo ya Olimpiki

Wachezaji wa timu ya taifa ya Kenya baada ya kushinda taji la irb series nchini Singapore
Wachezaji wa timu ya taifa ya Kenya baada ya kushinda taji la irb series nchini Singapore todayonline.com

Timu ya taifa ya Kenya ya mchezo wa raga kwa wachezaji saba kila upande imepangwa katika kundi moja na mabingwa wa dunia New Zealand, tayari kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil mwezi Agosti mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Mbali na New Zealand, Kenya pia itapambana na Uingereza na Japan katika kundi C.

Kenya inashiriki kwa mara ya kwanza katika michezo hii ya Olimpiki na mwezi Aprili iliishangaza dunia kwa kunyakua taji la IRB Series nchini Singapore, baada ya kuishinda Fiji.

Afrika Kusini imejumuishwa katika kundi la B na Australia, Ufaransa, Uhispania na Brazil.

Kundi A, kuna Fiji, Marekani, Argentina na Brazil.

Mechi hizo zitaanza tarehe 9 mwezi Agosti na kumalizika tarehe 11.