RIADHA-RIO

Bolt apata jeraha la paja, hatihati kushiriki michezo ya London na Rio

Wanariadha wa Jamaica walioshiriki mbio za kufuzu mita 100 mjini Kingston Jamaica, kutoka Kushoto Jevaughn Minzie, Usain Bolt, Senoj-Jay Givans na Dexter Lee wakati wakimaliza mbio za nusu fainali.
Wanariadha wa Jamaica walioshiriki mbio za kufuzu mita 100 mjini Kingston Jamaica, kutoka Kushoto Jevaughn Minzie, Usain Bolt, Senoj-Jay Givans na Dexter Lee wakati wakimaliza mbio za nusu fainali. REUTERS/Gilbert Bellamy

Bingwa mara tatu na mshindi wa medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki, Usain Bolt, amepata jeraha linaloweza kumfanya asishiriki michezo ya Rio, baada ya kuumia kwenye michezo ya majaribio ya wanariadha wa Jamaica.

Matangazo ya kibiashara

Bolt mwenye umri wa miaka 29, alipata maumivu ya msuli wakati wa raundi ya kwanza ya mbio za mita 100 na alijiondoa baada ya kushinda hatua ya nusu fainali ya majaribio ya wanariadha hao.

Hata hivyo licha ya kuumia, anatarajiwa kutetea nafasi yake kwenye mita 100 na 200 ili kuteuliwa kwenye timu ya taifa ya Jamaica, kwakuwa sera yao inaruhusu na kutoa upendeleo kwa wanariadha wanaopatia matibabu.

Daktari wa mwanariadha huyo, amesema Bolt anahitaji matibabu ya haraka na ni matumaini yake kuwa atarejea kwenye mbio za kumbukumbu ya michezo ya Olimpiki ya London, Julai 22 mwaka huu.

Katika michezo kadhaa ya dunia aliyoshindwa kushiriki, mshindi wa mbio za mita 100 raia wa Jamaica mjini Kingstone, zilishindwa na mshindi wa medali ya fedha mwaka 2012, Yohan Blake kwa muda wa sekunde 9.95.