EPL-MANUTD

Hatimaye Ryan Giggs atangaza kuachana na Man Utd

Aliyewahi kuwa mchezaji, kocha wa mpito na baadae kuwa kocha msaidizi chini ya Louis van Gaal, Ryan Giggs, ataachana na klabu yake aliyoitumikia kwa muda mrefu toka akiwa na umri wa miaka 14.

Aliyewahi kuwa kocha wa mpito na baadae kocha msaidizi wa klabu ya Manchester United, Ryan Giggs, ametangaza kuachana na timu hiyo baada ya miaka 29
Aliyewahi kuwa kocha wa mpito na baadae kocha msaidizi wa klabu ya Manchester United, Ryan Giggs, ametangaza kuachana na timu hiyo baada ya miaka 29 REUTERS/Darren Staples
Matangazo ya kibiashara

Taarifa za Giggs kuachana na United, zimekuja majuma kadhaa baada ya uwepo wa uvumi kuwa huenda akaachana na timu hiyo baada ya kuondoka kwa kocha van Gaal, na kuwasili kwa Jose Mourinho, ambapo sasa anasema anataka kupata nafasi ya kuwa kocha kamili.

Giggs mwenye umri wa miaka 42 hivi sasa, ndiye mchezaji pekee, aliyecheza mara nyingi zaidi kuliko mwingine yeyote, akiwa na klabu ya Manchester United, akitajwa kuwa mchezaji mwenye kipaji kuwahi kutokea na kushinda kila taji muhimu akiwa na timu yake.

Giggs mwenyewe amesema "Baada ya miaka 29 ndani ya klabu ya Manchester United kama mchezaji na kocha msaidizi, najua ushindi ni kinasaba cha hii klabu - kutoa nafasi kwa vijana, kucheza mchezo wa kushambulia na mpira wa kuvutia. Ni afya kuwa na matarajio makubwa, na nihaki kutarajia ushindi, Manchester United inatarajia, inastahili ba si zaidi.

Ryan Giggs wakati akiwa anaichezea timu yake ya Manchester United, sasa ametangaza kuchana nayo baada ya miaka 29 ya maisha yake na timu hiyo
Ryan Giggs wakati akiwa anaichezea timu yake ya Manchester United, sasa ametangaza kuchana nayo baada ya miaka 29 ya maisha yake na timu hiyo REUTERS/Nigel Roddis

"Ndio maana huu ni uamuzi mkubwa kuuchukua, kwangu mimi kuachana na klabu ambayo imekuwa maisha yangi toka nikiwa na miaka 14. Sio uamzi ambao nimeuchukua kirahisi. Nitachukua kumbukumbu nyingi pamoja na uzoefu wa maisha, na hivyo natarajia kupata mafanikio katika siku zijazo.

Nguli huyo wa Man Utd ameongeza kuwa "hata hivyo, nafikiri ni muda muafaka licha ya kuwa sina mipango ya karibu ya kuwa kocha lakini ni suala ambalo nalitaka sana.

Giggs amempongeza kocha Jose Mourinho kwa kuteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo na kwamba ni watu wachache wanaopata nafasi ya kuinoa klabu kubwa kama Man Utd lakini anaamini Mourinho ni chagua sahihi.