EURO 2016

Ujerumani na Italia patashika nguo kuchanika Euro 2016

Wachezaji wa Ujerumani wakimpongeza, Mario Gomez jezi namba 23, aliyeifungia timu yake bao la ushindi dhidi ya Ireland Kaskazini, 21 Juni 2016.
Wachezaji wa Ujerumani wakimpongeza, Mario Gomez jezi namba 23, aliyeifungia timu yake bao la ushindi dhidi ya Ireland Kaskazini, 21 Juni 2016. REUTERS/John SibleyLivepic

Michuano ya kombe la mataifa Ulaya imefikia pazuri baada ya kufahamika kwa timu mbili zitakazocheza kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya mwaka huu inayoelekea ukingoni nchini Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Jumamosi usiku, Julai 2, kutakuwa na mtanange wa mechi moja tu wa hatua ya robo fainali, ambapo timu ya taifa ya Ujerumani ambao ni mabingwa wa kombe la dunia lililopita nchini Brazil, watakuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Italia "The Azzuri".

Ujerumano inayonolewa na kocha Joachim Low, inaingia uwanjani kwenye mchezo huu, ikiwa na historia nzuri ya kuanza vyema michuano ya mwaka huu mpaka kwenye hatua waliyofikia baada ya kutopoteza mchezo hata mmoja.

Ujerumani inataka kutengeneza Historia ya kuwa timu nyingine itakayofanikiwa kutwaa taji la michuano ya Ulaya baada ya lile la kombe la dunia kama ilivyowahi kufanya timu ya taifa ya Hispania, iliyotwaa kombe la dunia mwaka 2010 na kushinda taji la Ulaya mwaka 2012.

Mlinda mlango wa Italia, Gianluig Buffon akimpngeza Graziano Pelle baada ya kuipatia timu yake bao la pili dhidi ya Ubelgiji 13 june 2016
Mlinda mlango wa Italia, Gianluig Buffon akimpngeza Graziano Pelle baada ya kuipatia timu yake bao la pili dhidi ya Ubelgiji 13 june 2016 REUTERS/Jason Cairnduff Livepic

Italia inayonolewa na kocha, Antonio Conte, inaingia kwenye mchezo huu, ikiwa pia na rekodi nzuri ya ukuta wake kutopitika kwa urais wala kuruhusu mabao mengi, huku wakiwa na kumbukumbu ya kuifunga Uhispania na kuitupa nje timu hiyo kwenye hatua ya 16 bora.

Mario Gotze wa Ujerumano na Pelle wa Italia ni wachezaji wanaotazamwa sana kwenye mchezo huu kutokana na mchango wao kwenye vikosi vya timu zote mbili.

Siku ya Ijumaa, Wales walifanikiwa kuweka hostoria kwa kufika kwa mara ya kwanza kwenye hatua ya makundi kwenye michuano mikubwa duniani, baada ya kuchomoza na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ubelgiji.

Kwa matokeo hayo sasa, Wales watacheza hatua ya nusu fainali na timu ya taifa ya Ureno.