EURO 2016-UFARANSA-ICELAND

Euro 2016: Ufaransa yaibwaga Iceland sasa kucheza na Ujerumani

Les Beus washerehekea bao la Antoine Griezmann katika mechi kati ya Ufaransa na Iceland, Euro 2016.
Les Beus washerehekea bao la Antoine Griezmann katika mechi kati ya Ufaransa na Iceland, Euro 2016. REUTERS/Carl Recine Livepic

Timu ya soka ya Ufaransa itamenyana na ile ya Ujerumani katika mchuano wa nusu fainali wa michuano ya Kombe la mataifa ya Ulaya (Euro 2016) Julai 7 katika uwanja wa mpira wa Marseille.

Matangazo ya kibiashara

Ufaransa wamemaliza mechi yao kwa mafanikio zaidi dhidi ya Iceland kwa kuiburuza mabao 5-2, Jumapili hii Julai 3 katika uwanja wa mpira wa Saint-Denis, katika mechi ya robo fainali.

Ushindi huo ni wa kwanza kwa timu ya ufaransa tangu kuanza kwa michuano ya Kombe la mataifa ya Ulaya kwa kufunga mabao matano katika mechi tu moja. Jambo jingine lililowashangaza wengi hasa mashabiki wa timu hiyo kuona karibu mabao yote ikiyapata katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Bao la kwanza la Ufaransa lilifungwa katika dakika ya 12, kupitia mchezaji Olivier Giroud. Mshambuliaji huyu wa timu ya taifa ya soka ya Ufaransa , alifanikiwa kuweka mpira wavuni baada ya mpira aliyokuwa amepewa kutoka kwa Blaise Matuidi kujogonga kwenye mgongo wa wa beki wa Iceland, na hivyo Ufaransa kuandikisha bao (1-0). Dakika nane baadaye Paul Pogba hakuchelewa kuipatishia timu yake nbao la pili katika dakika ya 20, baada ya mkwaju wa kona uliyopigwa na Antoine Griezmann.

Anotine Griezmann aonyesha maajabu yake

Antoine Griezmann alihusika pia katika kuifungia timu yake mabao mawili. Katika dakika ya 43, ushupavu wake ulipelekea Dimitri Payet kupata nafasi nzuri ya kufunga bao la tatu 3-0.

Kwa muda wa dakika 45 za kipindi cha kwanza Ufaransa ilijikua ikiiburuza Iceland kwa mabao 4-0.

Itafahamika kwa timu hii ya Iceland, iliiondoa timu ya taifa ya soka ya Uingereza katika mechi za mtoano
Ufaransa inajiandaa kumenya katika mechi ya nusu fainali na Ujerumani, mechi ambayo itapigwa Alhamisi Julai 7

EURO 2016: nusu fainali

Ureno kucheza na Wales, Jumatano, Julai 6 saa 1 usiku saa za kimataifa katika uwanja wa mjini Lyon

Ijerumani kupambana na Ufaransa, Alhamisi Julai 7 saa 1 saa za kimataifa katika uwanja wa mjini Marseille.

Fainali ya michuano ya Kombe la mataifa ya Ulaya (Euro 2016) itachezwa Jumapili Julai 10 saa 1 saa za kimataifa katika uwanja wa mjini Saint-Denis.