SOKA

Jorge Costa afutwa kazi kama kocha wa Gabon

Kocha wa Gabon  Jorge Costa
Kocha wa Gabon Jorge Costa www.maisfutebol.iol.pt.gif

Shirikisho la soka nchini Gabon limetangaza kumfuta kazi kocha wa timu ya taifa Jorge Costa.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja miezi sita kabla ya nchi hiyo ya Afrika ya Kati kuwa mwenyeji wa michuano ya mataifa bingwa barani Afrika.

Raia huyo wa Ureno, alianza kazi ya kuifunza Gabon mwaka 2014.

Aidha, kufutwa kazi kwa kocha huyu kunakuja baada ya Gabon kupangwa pamoja na Ivory Coast, Mali na Morocco katika kundi moja kufuzu katika kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Costa alikuwa kocha aliyelipwa mshahara mkubwa kama kocha wa timu ya bara la Afrika.

Mwezi Mei mwaka huu, kocha huyo alibaini kuwa analipwa Euro 70,000 akiwa ana maana kuwa ndiye kocha bora barani Afrika.

Mechi ya mwisho aliyoingoza ilikuwa ni kati ya Gabon na Ivory Coast katika mchuano wa kirafiki na kufungwa mabao 2 kwa 1.

Kocha mpya wa Gabon anatarajiwa kutajwa mwisho wa mwezi huu.