SOKA-TANZANIA

Msemaji wa klabu ya Yanga FC aadhibiwa na TFF

Msemaji wa klabu ya Yanga Jerry Muro
Msemaji wa klabu ya Yanga Jerry Muro Yanga FC

Kamati ya maadili ya Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limemfungia mwaka mmoja na kumtoza faini msemaji wa klabu ya Yanga FC, Jerry Muro.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imekuja baada ya Kamati hiyo kusema kuwa msemaji hiyo amepatikana na kosa la kupinga maamuzi ya TFF kuhusu haki za matangazo ya Televisheni lakini pia kutumia lugha mbaya kabla ya mchuano wa Shirikisho barani Afrika kati ya kati Yanga na TP Mazembe mwezi uliopita.

Kosa lingine pia ni kuwashawishi mashabiki wa Yanga kuwafanyia vurugu mashabiki wa Simba kwenye mchezo huo ambao timu yake ilifungwa 1-0.

Adhabu hii inamaanisha kuwa hatajihusisha na maswala ya soka kwa muda huo lakini pia ametozwa fainali ya Shilingi za Tanzania Milioni 3.

Wakati wa hukumu hiyo, Muro hakuwepo kwenye kikao hicho cha maamuzi.