EURO 2016-UFARANSA-URENO

Ureno wachukua ubingwa Ulaya 2016

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Ureno, Fernando Santos, akinyanyuliwa na wachezaji wake baada ya ushindi katika fainali ya Euro 2016.
Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Ureno, Fernando Santos, akinyanyuliwa na wachezaji wake baada ya ushindi katika fainali ya Euro 2016. REUTERS/Kai Pfaffenbach Livepic

Ureno wameshinda michuano ya Kombe la Ulaya (Euro 2016) kwa kuifua Ufaransa, ambao ni wenyeji wa michuano hiyo kwa bao 1-0. Timu zote mbili zilimaliza mchezo kiwa sare ya kutofungana.

Matangazo ya kibiashara

Bao la ureno limeingizwa katika dakika za ziada na Eder katika dakika ya 110 ya mchezo wa fainali mjini Paris.

Wachezaji na mashabiki wa timu ya soka ya Ufaransa wamepata huzuni mkubwa kwa kufungwa na Ureno licha ya kutoka sare katika dakika zote tisini za mchezo wa kawaida
Mechi kati ya Ufaransa na Ureno ilipigwa katika uwanja wa Stade de France. Ufaransa ilitawala mchezo kwa kiasi kikubwa, lakini hawakuweza kuzitumia vyema nafasi walizopata.

Hata hivyo Ureno walicheza kwa kujituma na ushirikiano. Katika mchezo huo mchezaji nyota wa timu hiyo Cristiano Ronaldo hakubahatika kumaliza dakika zote tisini za mchezo. Aliondolewa uwanjani baada ya kupata jeraha la goti katika kipindi cha kwanza.

Hii ni mara ya kwanza Ureno kushinda michuano mikubwa kama hii.