DEMBA BA

Ba huenda asirudi tena uwanjani baada ya kuvunjika mguu

Mchezaji wa klabu ya Shanghai Shenhua, Demba Ba, ambaye mwishoni mwa juma alivunjika mguu kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uchina
Mchezaji wa klabu ya Shanghai Shenhua, Demba Ba, ambaye mwishoni mwa juma alivunjika mguu kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uchina DR

Mshambuliaji wa zamani kwenye ligi kuu ya nchini Uingereza, Demba Ba, amepata jeraha la kuvunjika mkuu, ambalo huenda likamsababisha kustaafu soka, wakati akichezea timu yake kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uchina, Super League. 

Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji huyo wa kimataifa raia wa Senegal, alizimia baada ya kugongana na mchezaji mwingine, ambapo mguu wake wa kushoto ulivunjika kabisa, eneo jirani na goti lake la kushoto.

Tukio hili lilijiri wakati timu yake ya Shangai Shenhua ilikuwa ikipepetana na mahasimu wao Shanghai SIPG, siku ya Jumapili.

Kocha mkuu wa klabu ya Shanghai Shenhua, Gregorio Manzano, amewaambia waandishi wa habari maea baada ya mchezo huo kuwa, huenda jera alilolipata Demba Ba, likawa limehitimisha maisha yake ya soka.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya West Ham, Newcastle na Chelsea, alijiunga na klabu hiyo ya Uchina akitokea klabu ya Besiktas ya Uturuki kwa dau la paundi milioni 12 za Uingereza, mwezi Julai mwaka jana.

Mpaka anavunjika mguu, Ba alikuwa anaongoza kwenye safu ya wachezaji wenye mabao mengi, ambapo alikuwa na mabao 14 katika mechi 18 ambazo amecheza hadi sasa.