BRAZIL-MICHEZO YA OLIMPIKI

Brazil yaimarisha usalama wake ikikaribia Michezo ya Olimpiki

Wanajeshi na askari polisi 85 000 watawekwa katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha usalama wa Michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro.
Wanajeshi na askari polisi 85 000 watawekwa katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha usalama wa Michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro. REUTERS/Bruno Kelly

Baada ya shambulizi la mjini Nice Julai 14, serikali ya Brazil imeimarisha hatua za usalama wake, siku 20 kabla ya kuanza kwa Michezo ya Olimpiki katika mji wa Rio de Janeiro.

Matangazo ya kibiashara

Siku tatu baada ya shambulizi la mjini Nice, siku 20 kabla ya kuanza kwa Michezo ya Olimpiki ya mjini Rio, Brazil imetangaza kuimarisha usalama kwa minajili ya Michezohiyo. Uamuzi huu ulichukuliwa Ijumaa Julai 15 baada ya mkutano wa kilele uliyoongozwa na Rais wa mpito Michel Temer. Serikali ya Barazil ililikuwa ilitangaza kabla hata ya mkutano huo kwamba uimarishwaji wa usalama utahusu vituo vya ukaguzi. Wasiwasi kuhusu Michezo ya Olimpiki "umeongezeka siku za hivi karibuni" baada ya shambulio katika mji wa Nice, nchini Ufaransa, alikiri afisa wa Idara ya Ujasusi ya Brazil, Sergio Etchegoyen.

Udhibiti waimarishwa kwa safari za ndege za ndani kuanzia Jumatatu Julai 18

Baadhi ya barabara zitafungwa na magari yasio na ruhusa yatanyimwa haki ya kuingia karibu na maeneo manne ambapo Michzo ya Olimpiki iatendeshwa. Ukaguzi wa abiria na mizigo yao kwa safari za ndege za ndani utaimarishwa kuanzia Jumatatu hii Julai 18 katika viwanja vyote vya ndege nchini Brazil. Mamlaka ya safari za anga nchini Brazil imehakikisha kwamba mabadiliko haya yanahusu tu "kuweka sawa viwango vya usalama".

ulipuaji wa shambulio la bomu Jumamosi katika kituo cha treni mjini Rio ulikuwa na mafanikio. "Zoezi muhimu," kwa mujibu wa jeshi, hata kama ilikuwa, kwa mujibu wa afisa mmoja wa ngazi ya juu katika jeshi la Brazil, mafunzo zaidi miongoni mwa yale yaliyotekelezwa, na ilikua imeshatolewa tahadhari kabla ya mauaji ya mjini Nice. "Hakuna tishio thabiti dhidi ya Brazil," amesema afisa wa usalama wa Michezo. Kiwango cha tahadhari ya nchi kiko kwenye rangi ya njano.

Usalama kuimarishwa kwa wanariadha wa Ufaransa

Lakini katika ripoti ya tume ya uchunguzi ya Bunge la Ufaransa kuhusu mashambulizi yaliyotekelezwa katika mji wa Paris mwaka 2015, iliyotolewa wiki hii, Mkuu wa Idara ya Upelelezi katika jeshi la faransa a,ebaini kwamba kulikuwepo na mpango wa shambulizi dhidi ya wanariadha wa Ufaransa katika Michezo hiyi ya Olimpiki. Afisa mwandamizi wa Idara ya Upelelezi wa Brazil anatarajiwa Jumatatu hii mjini Paris kujadili suala hilo. Serikali ya Brazil tayari imehkikisha kwamba ulinzi utaimarishwa kwa baadhi wajumbe, ikiwa ni pamoja na wale wa Ufaransa na Marekani.

Wanajeshi na askari polisi 85,000 watatumbwa katika maeneo mbalimbali wakati wa Michezo ya Olimpiki kwa usalama wa wanariadha na watalii 500,000 kutoka duniani kote wanatarajiwa kushiriki michuano hiyo.