WADA-URUSI

Ripoti mpya yaididimiza Urusi kufuatia madawa yanayosisimua mwili

Mwandishi wa ripoti, Richard McLaren, katika mkutano na waandishi wa habari, Jumatatu, Julai 18, 2016.
Mwandishi wa ripoti, Richard McLaren, katika mkutano na waandishi wa habari, Jumatatu, Julai 18, 2016. REUTERS/Peter Power

Richard McLaren, ambaye aliongoza uchunguzi huru, anasema katika ripoti iliofanywa kwa agizo la Shirika linalopambana na madawa ya kusisimua mwili (WADA) na kutolewa Jumatatu Julai 18, jinsi Urusi ilivyobuni "mfumo salama wa Serikali wa matumizi ya madawa ya kusisimua mwili" katika michezo ya Olimpiki ya Sochi mwaka 2014.

Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi huru uliendeshwa na Daktari Richard McLaren, kutoka Canada unabaini mbinu ya kufungua chupa za kubeba mkojo na kubadilisha mikojo.

Uchunguzi wake ulibaini kuwa asilimia 100% ya chupa hizo za mikojo zilikuwa na dalili za kufunguliwa kabla na baada ya michezo ya msimu wa baridi ya Sochi mwaka wa 2014.

Uchungzi huo utaipa shinikizo kamati ya kimataifa ya olimpiki kukipiga marufuku kikosi chote cha Urusi kutoka kwa mashindano ya olimpiki ya mjini Rio ambayo yatafanyika china ya majuma matatu yanayokuja.

Baada kashfa ya rushwa na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini, suala lililoibua masuala mengi katika Shirikisho lake ka Riadha, Urusi inakabiliwa tena na shutma za matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini. Urusi ilikua na mpango wa kisiri ya kutoa madawa ya kuongeza nguvu mwilini kwa wanariadha yake walioshindana mashindano ya msimu wa baridi ya Sochi.

Katika ripoti iliyotolewa Jumatatu hii, ni wazi kwamba maabara yanayopambana dhidi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini ya Urusi na Sochi yaliwalindia siri wanariadha wa Urusi waliokua walitumia madawa ya kusisimua mwili, katika sehemu ya "mfumo salama wa Serikali wa matumizi ya madawa ya kusisimua mwili", uliyoongozwa, kudhibitiwa na kusimamiwa" na Wizara ya Michezo ya Urusi, "kwa msaada wa Idara ya Ujasusi ya Urusi (FSB).