OLIMPIKI-BRAZIL 2016

Burundi mbioni kutafuta medali yake ya pili nchini Brazil

Burundi itawakilishwa na wanamichezo saba katika michezo ya Olimpiki nchini Brazil itakayoanza tarehe 5 mwezi ujao.

Mwanariadha wa Burundi Diane Nukuri
Mwanariadha wa Burundi Diane Nukuri boulderwave.com
Matangazo ya kibiashara

Haya ni makala ya tano kwa Burundi kushiriki katika michuano hii mwaka 1996, 2000, 2004, 2008, 2012 na 2016.

Nchi hiyo itawakilishwa katika michezo miwili, riadha na Judo.

Olivier Irabaruta ataiwakilisha nchi yake katika mbio za Mita 10000 na 5000 kwa upande wa wanaume.

Pierre Celestin Nihorimbere na Abraham Niyonkuru nao watapambana katika mbio za Marathon kwa wanaume, kujaribu kuitafutia nchi yake medali.

Diane Nukuri ambaye alikimbilia uhamishoni nchini Canada, naye atashiriki katika mbio za Mita 10000 kwa wanawake na Marathon pia kwa upande wa wanaume.

Francine Niyonsaba atashiriki mbio za Mita 800 kwa wanawake huku Antoine Gakeme akiwakilisha nchi yake katika mbio za Mita 800 kwa upande wa wanaume.

Mbali na riadha, Antoinette Gasongo ni mchezaji pekee atayeiwakilisha nchi yake katika mchezo wa Judo kwa upande wa wanawake kwenye uzani wa kilo 52.

Katika historia ya michezo hii, Burundi imeshinda tu medali moja ambayo ni ya dhahabu mwaka 1996 wakati michezo hii ilipofanyika Atlanta nchini Marekani kupitia mwanariadha Venuste Niyongabo aliyeshinda mbio za Mita 5000 kwa upande wa wanaume.