Jukwaa la Michezo

CECAFA haijapata mwenyeji wa michuano ya klabu bingwa mwaka 2016

Imechapishwa:

Baraza la soka Afrika Mashariki na Kati CECAFA, bado halijapata mwenyeji wa michuano ya mwaka huu kuwania taji la Kagame, ambalo lilikuwa limepangwa kufanyika kati ya tarehe 18 mwezi Juni na kumalizika mwezi Julai tarehe 2 nchini Tanzania.Shirikisho la soka nchini Tanzania lilikataa kuwa wenyeji wa makala haya ya 41, kwa kile walichokisema kuwa ilikuwa na michuano ya Kimataifa huku nchi za Sudan na Rwanda ambazo zilikuwa zimeombwa kuchuku nafasi zikisalia kimya hadi sasa.

Mabingwa wa mwaka 2015 wa CECAFA Azam FC kutoka Tanzania
Mabingwa wa mwaka 2015 wa CECAFA Azam FC kutoka Tanzania CECAFA
Vipindi vingine