FIFA

Bara la Afrika kupata nafasi mbili zaidi kombe la dunia mwaka 2026

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino
Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino FIFA

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino, ametangaza kuwa bara la Afrika litapata nafasi mbili zaidi wakati wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2026.

Matangazo ya kibiashara

Hii ina maana kuwa bara la Afrika litawakilishwa na mataifa 7 kutoka 5 kama ilivyo sasa,na  mataifa yatakayoshiriki yatakuwa ni 40 badala ya 32 kama ilivyo sasa.

Infantino ametoa ahadi hii katika mkutano wake na viongozi wa vyama vya soka barani Afrika, jijini Abuja nchini Nigeria.

Wakati wa kampeni kutafuta urais wa FIFA mapema mwaka huu, Infantino aliahidi kuongeza mataifa yanayoshiriki katika kombe la dunia kufikia 40 kipindi cha uongozi wake.

Hata hivyo, hili litafikiwa tu ikiwa mapendekezo yake kwa viongozi wa mashirikisho la soka duniani, yatakubali katika mkutano mkuu wa FIFA.

Michuano ijayo ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi na 2022 nchini Qatar itakuwa na mataifa 32.