CAF-SOKA

Bitily ateuliwa kuongoza umoja wa vyama vya soka kutoka Mataifa yanayozungumza Kiingereza

Rais wa Shirikisho la soka nchini Liberia Musa Bitily ameteuliwa na viongozi wenzake kutoka mataifa yanayozungumza lugha ya Kiingereza barani Afrika, kuongoza umoja wenye ajenda ya kuimarisha mchezo wa soka barani Afrika.

Musa Bitily rais wa Shirikisho la soka nchini Liberia
Musa Bitily rais wa Shirikisho la soka nchini Liberia ckoment
Matangazo ya kibiashara

Uteuzi huo umefanyika jijini Abuja nchini Nigeria baada ya viongozi 19 kutoka mataifa hayo ya Afrika kukutana kando ya kikao rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino aliyezuru nchi hiyo wiki hii.

Akijibu maswali kutoka kwa wadau wa soka wakiwemo wanahabari wa mchezo wa soka barani Afrika kupitia kundi la Football Africa Arena, Bitily ambaye aliwahi kuonesha nia ya kuwania urais lakini ndoto yake ikakatizwa na uongozi wa CAF, amesisistiza kuwa umoja wao ni wa kuleta mawazo yao pamoja kuinua soka.

“Umoja huu unalenga kusaidia kusukuma ajenda ya kuleta mabadiliko katika mchezo wa soka hapa barani Afrika, “ alisema.

Aidha, ameongeza kuwa umoja huo utawasaidia kuzungumza kwa sauti moja kuhusu maswala mbalimbali ya soka na kuhakikisha kuwa maslahi yao yanatekelezwa.

“Hatutakubali kutishwa na yeyote, tunafahamu kuwa tuna kiongozo wetu Issa Hayatou ambaye ni rais wa CAF na tutashirikiana naye,” aliongeza.

Umoja huu unakuja huku uongozi wa juu wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF, ukiendelea kuwakilishwa na watu kutoka mataifa yanayozungumza Kifaransa na Kiarabu kwa muda mrefu.

 

Viongozi hao ni pamoja na :-Issa Hayatou-Rais kutoka Cameroon.

Suketu Patel-Makamu wa kwanza wa rais wa kwanza kutoka Ushelisheli.

Almamy Kabele Camara-Makamu wa pili wa rais kutoka Guinea

Hicham El Amrani-Katibu Mkuu kutoka Morocco.

Mohamed El Sherei-Mwekahazina kutoka Misri.

Viongozi hao ambao walikutana na kuuunda Umoja huo ni pamoja na:-Kwesi Nyantakyi (Ghana), Lamin Kaba Bajo (The Gambia), Isha Johansen (Sierra Leone), Musa Bility (Liberia), Juneidi Basha Tilmo (Ethiopia), Nick Mwendwa (Kenya), Andrew Chamanga(Zambia).

Wengine ni pamoja na:- Philip Chiyangwa (Zimbabwe), Frans Mbidi (Namibia), Chabur Goc Alei (South Sudan), Walter Nyamilandu (Malawi), Abdiqani Said Arab (Somalia), Vincent Nzamwita (Rwanda), Moses Magogo (Uganda), Jamal Malinzi (Tanzania), Augustin Senghor (Senegal) and Souleman Waberi (Djibouti).