CAF-SOKA

TP Mazembe yaikaribisha MO Bejaia mjini Lubumbashi

cafonline

Michuano ya soka kuwania taji la klabu bingwa na Shirikisho barani Afrika inaendelea leo katika mataifa mbambali.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni michuano ya nne ikiwa ni hatua ya makundi katika michuano hii inayochezwa nyumbani na ugenini.

TP Mazembe ya DRC ambayo msimu huu inatafuta ubingwa wa taji la Shirikisho ni wenyeji wa klabu ya MO Bejaia ya Algeria mjini Lubumbashi.

Mazembe inaongoza kundi la A kwa alama 7 baada kupata ushindi mara mbili na kwenda sare ya kutofungana.

Wiki iliyopita, Mazembe ilitoka sare ya kutofungana na MO Bejaia katika mchuano kwa kwanza ugenini.

MO Bejaia na Medeama ya Ghana hadi sasa zina alama 5 huku matumaini ya klabu ya Yanga FC ya Tanzania kusonga mbele yakididimia baada ya kufungwa hapo jana na Medeama kwa mabao 3 kwa 1 ugenini.

Yanga yenye makao yake jijini Dar es salaam sasa imesalia na mechi mbili, kati ya MO Bejaia nyumbani na TP Mazembe ugenini mwezi ujao.

Matokeo ya kundi B
Al-Ahli Tripoli (Libya) 0-Etoile du Sahel (Tunisi) 1
Mechi ya leo

FUS Rabat (Morroco) vs Kawkab Marrakech(Morocco)

Ratiba ya michuano ya klabu bingwa
Kundi A

ASEC Mimosas (Cote Dvoire) vs ZESCO United (ZAMBIA)
Wydad Casablanca (Morroco) vs Al-Ahly (Misri)
Kundi B
Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) vs Zamalek (Misri).