Rio 2016-URUSI

RIO-2016: wanariadha wa Urusi wawasili Rio

Mashindano ya Michezo ya Olimpiki yaanza katika mji wa Río de Janeiro Agosti 5-21.
Mashindano ya Michezo ya Olimpiki yaanza katika mji wa Río de Janeiro Agosti 5-21. REUTERS/Ricardo Moraes

Wanariadha kadhaa wa Urusi wamewasili Alhamisi katika mji wa Rio de Janeiro, wakiruhusiwa na mashirikisho yao ya kimataifa kwa kushiriki katika michezo ya Olimpiki-2016 (Agosti 05-21) tofauti na Warusi watatu ambao wangelishiriki katika mashindano ya mbio za baiskeli, baada ya kutengwa kwao katika mashindano hayo.

Matangazo ya kibiashara

"Kwa upande wa madawa ya kusisimua mwili, tunajaribu kusahihisha tatizo hilo na tunaweza kusema kwamba wanariadha wasafi pekee ndio wamewasili hapa leo" (Alhamisi), amesema Yuri Butnev, msemaji wa Kamati ya Michezo ya Olimpiki ya Urusi (ROC), alipokua akishuka akitoka ndani ya ndege.

wanariadha walipokelewa katika uwanja wa ndege wa Rio de Janeiro na raia wa Urusi waliokuja kuhudhuria mashindano hayo. "Ni lazima tuwaunge mkono mara mbili kwa sababu ya historia hii, timu yetu itakuwa na nguvu," amesema Anatoly Saving.

Rais wa Kamati ya Michezo ya Olimpiki nchini Urusi, Alexander Zhukov, alikua aliongozana Alhamisi hii asubuhi na wanariadhaa wake hadi kwenye uwanja wa ndege wa Moscow, ili kuwapa faraja na nasaha za mwisho, akiwataka kuonyesha ujasiri kwa manufaa ya taifa la Urusi.