Jukwaa la Michezo

Umoja wa vyama vya soka kutoka Mataifa yanayozungumza Kiingereza waundwa

Sauti 21:10
Marais wa marais 19 kutoka bara la Afrika wakikutana na rais wa FIFA Gianni Infatinno jijini Abuja
Marais wa marais 19 kutoka bara la Afrika wakikutana na rais wa FIFA Gianni Infatinno jijini Abuja FIFA.COM

Rais wa Shirikisho la soka nchini Liberia Musa Bitily ameteuliwa na viongozi wenzake kutoka mataifa yanayozungumza lugha ya Kiingereza barani Afrika, kuongoza umoja wenye ajenda ya kuimarisha mchezo wa soka barani Afrika.Uteuzi huo umefanyika jijini Abuja nchini Nigeria baada ya viongozi 19 kutoka mataifa hayo ya Afrika kukutana kando ya kikao rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino aliyezuru nchi hiyo wiki hii.