URUSI-CIO

RIO-2016: Bodi ya IOC kujadili orodha ya Warusi wataoruhusiwa katika mashindano

Wanariadha wanyoosha misuli katika uwanja wa Nagai mjini Osaka.
Wanariadha wanyoosha misuli katika uwanja wa Nagai mjini Osaka. (Photo: AFP)

Siku tatu kabla ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki, vigogo wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) wanakutana kuanzia Jumanne katika mji wa Rio de Janeiro, katika hali ya mvutano kuhusu hatima ya wanariadha wa Urusi, ambao kukata rufaa mbele ya Mahakama ya usuluhishi ya Michezo (CAS).

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya wanariadha wa Urusi walioruhusiwa kushiriki katika michezo ya Olimpiki ya mjini Rio de Janeiro, kuanzia Ijumaa, Agosti 5, inaweza kutolewa baada ya kikao hiki, amesema Jumatatu Waziri wa Michezo wa Urusi, Vitaly Mutko, ambapo nchi yake inakabiliwa na shutuma za matumizi ya madawa ya kusisimua mwili.

"Natumaini kwamba leo au kesho, taratibu zote zitakazopelekea timu yetu [kushiriki mashindano ya mjini Rio] zitakua zimekamilika," Waziri Vitaly Mutko amesema mjini Paris, kwa mujibu wa taarifa iliyonukuliwa n shirika la habari la Urusi Ria Novosti.

Itafahamika kwamba wanariadha kadhaa wa Urusi waliwasili Alhamisi juma lililopita katika mji wa Rio de Janeiro, wakiruhusiwa na mashirikisho yao ya kimataifa kwa kushiriki katika michezo ya Olimpiki-2016 (Agosti 05-21) tofauti na Warusi watatu ambao wangelishiriki katika mashindano ya mbio za baiskeli, baada ya kutengwa katika mashindano hayo.

"Kwa upande wa madawa ya kusisimua mwili, tunajaribu kusahihisha tatizo hilo na tunaweza kusema kwamba wanariadha wasafi pekee ndio wamewasili hapa leo" (Alhamisi), alisema Yuri Butnev, msemaji wa Kamati ya Michezo ya Olimpiki ya Urusi (ROC), alipokua akishuka akitoka ndani ya ndege.

Wanariadha walipokelewa katika uwanja wa ndege wa Rio de Janeiro na raia wa Urusi waliokuja kuhudhuria mashindano hayo. "Ni lazima tuwaunge mkono mara mbili kwa sababu ya historia hii, timu yetu itakuwa na nguvu," alisema Anatoly Saving.

Rais wa Kamati ya Michezo ya Olimpiki nchini Urusi, Alexander Zhukov, alikua aliongozana Alhamisi hii asubuhi na wanariadhaa wake hadi kwenye uwanja wa ndege wa Moscow, ili kuwapa faraja na nasaha za mwisho, akiwataka kuonyesha ujasiri kwa manufaa ya taifa la Urusi.