SOKA

Nigeria kusaka ushindi wa pili michezo ya Olimpiki

Nwanko Kanu akisherehekea baada ya Nigeria kushinda fainali ya Michezo ya Olimpiki mwaka 1996
Nwanko Kanu akisherehekea baada ya Nigeria kushinda fainali ya Michezo ya Olimpiki mwaka 1996

Timu za taifa za soka za Nigeria na Cameroon zinasalia katika vitabu vya historia kuwa mataifa pekee ya Afrika kuwahi kushinda taji la Michezo ya Olimpiki katika mchezo wa soka kwa upande wa wanaume.

Matangazo ya kibiashara

Mwaka 1996 wakati michezo hii ilipofanyika nchini Marekani, kikosi cha Nigeria kilifika katika hatua ya fainali na kuifunga Argentina mabao 3 kwa 2.

Wakati wa michuano hiyo, Nigeria ilishinda mechi 5 na kufungwa mechi moja.

Wachezaji wa Nigeria walioshiriki katika fainali hiyo ni pamoja na Emmanuel Babayaro, Celestine Babayaro, Taribo West, Nwankwo Kanu, Jay Jaky Okocha, Daniel Amokachi , Sunday Oliseh miogoni mwa wengine.

Mwaka 2000, wakati michezo hii ilipofanyika nchini Australia, Cameroon nayo ilipata ushindi baada ya kuifunga Uhispania mabao 5 kwa 3 kupitia mikwaju ya penalti baada ya kupata sare ya mabao 2 kwa 2 katika muda wa kawaida na ule wa ziada.

Baadhi ya wachezaji walioiwakilisha Cameroon katika michezo hiyo ni pamoja na:- Samuel Eto'o,Patrick Mboma, Geremi, Serge Mimpo, Albert Meyong miongoni mwa wengine.

Swali ni je, bara la Afrika mwaka huu linaingia tena kwenye vitabu vya historia huko Brazil ? Inawakilishwa na Algeria, Nigeria na Afrika Kusini.