SOKA

Manchester United yakaribia kumsajili Paul Pogba

Paul Pogba
Paul Pogba fssta

Klabu ya soka ya Uingereza, Manchester United iko mbioni kumsajili Paul Pogba kutoka klabu ya Juventus ya Italia.

Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23, anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya wiki ijayo.

Pogba anarejea katika klabu yake ya zamani baada ya kuondoka mwaka 2012.

Ripoti zinasema kurejea kwake Old Trafford huenda kukawa ni usajili mkubwa sana kwa klabu hiyo msimu huu na hata kupita ule wa Gareth Bale mwaka 2013 alipouzwa kwa kima cha Pauni Milioni 85 katika klabu ya Real Madrid.

Utakuwa ni usajili wa nne wa kocha Jose Mourinho baada ya kumsajili Eric Bailly, Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan.

Ligi kuu ya soka nchini Uingereza inaanza Jumapili ijayo na United watafungua mechi yao ya kwanza dhidi ya Bournemouth.