SOKA

Kenya yapata kipigo cha mabao 7-0 kutoka kwa Cameroon

Kikosi cha timu ya taifa ya Kenya kisichozidi miaka 17
Kikosi cha timu ya taifa ya Kenya kisichozidi miaka 17 Sportpesanews.com

Timu ya taifa ya soka ya Kenya yenye chini ya umri wa miaka 17, ilianza vibaya safari ya kufuzu kucheza fainali ya Afrika mwaka ujao nchini Madagascar baada ya kufungwa mabao 7 kwa 0 na Cameroon mwishoni mwa wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Matokeo haya mabaya kutoka ugenini yanamaanisha kuwa Kenya ina kazi kubwa ya kujaribu kuyabadilisha wakati wa mchuano wa marudiano hivi karibuni jijini Nairobi.

Cameroon waliutawala mchezo huo na kuwazidi wageni wao katika idara zote.

Matokeo mengine ya mwishoni mwa wiki iliyopita:-

  • Mauritius 0 Angola 1
  • Zambia 0 Sudan 0
  • Ghana 5 Burkina Faso 1
  • Benin 1 Cote d'Ivoire 1
  • Tunisia 2 Senegal 3
  • Guinea 1 Morocco 1
  • Algeria 0 Gabon 0
  • Afrika Kusini 1 Tanzania 1
  • Misri 1 Ethiopia 3

Mataifa 8 yatafuzu katika fainali hiyo ya bara Afrika itakayofanyika kati ya tarehe 2 na 16 mwezi Aprili mwakani.

Mataifa manne yatakayofika katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo yatafuzu kucheza kombe la dunia kwa vijana nchini India baadaye mwaka ujao.