IBRAHIMOVIC-MAN UTD-EPL

Ibrahimovic: Mimi sina kiburi na wala sijivuni

Mshambuliaji mpya wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic akishangilia moja ya goli alilofunga wakati wa mchezo wa ngao ya Hisani hivi karibuni.
Mshambuliaji mpya wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic akishangilia moja ya goli alilofunga wakati wa mchezo wa ngao ya Hisani hivi karibuni. Reuters / Eddie Keogh Livepic

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza, Mswisi, Zlatan Ibrahimovic, amesema tuhuma dhidi yake kuwa ni mjivuni sio za haki na kwamba ujivuni wake ni kujiamini na anachokifanya. 

Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji huyu wa kimataifa wa Uswis, ambaye huenda akacheza mechi yake ya kwanza siku ya Jumapili kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Bournemouth, anafahamika kwa kujitweza na kujiona zaidi ya wapinzani wake.

Lakini hata hivyo, Zlatan mwenye umri wa miaka 34, anasema tabia yake inaakisi kile ambacho anakifanya uwanjani na ndio maana anaweza kushinda mataji mengi akiwa katika nchi nne tofauti, huku akipata nishani kemekem za heshima.

"Siamini kama nna kiburi kama vile watu wanavyofikiri," Zlatan amesema haya katika mahojiano maalumu na kituo cha Sky Sports cha nchini Uingereza.

"Nina jiamini. Naamini nachokifanya. Hivi sio kuwa mjivuni. Hiki ni kitu ninachoamini kuwa nguvu ya mtu na binadamu yeyote."

Mshambuliaji huyo ameongeza kuwa "mimi ni mtu wa kawaida. Watu wanayo picha yangu kuwa ni mtu mbaya, niko hivi niko vile. Watu wana shahuku: Huyu Zlatan yukoje?'

"Mimi ni mtu wa familia. Ninaijali familia yangu, lakini ninapokuwa uwanjani nina kuwa Simba. Hiyo ndio tofauti kubwa." alimaliza Zlatan.