Kenya yapata medali ya kwanza ya dhahabu katika mbio za Marathon kwa wanawake

Sauti 21:45
Jemima Sumgong asherehekea ushindi wa mbio za Marathon Jumapili Agosti 14 2016 nchini Brazil
Jemima Sumgong asherehekea ushindi wa mbio za Marathon Jumapili Agosti 14 2016 nchini Brazil Daily Nation

Mwanariadha Jemima Sumgong kutoka nchini Kenya, aliishindia  nchi yake medali ya kwanza ya dhahabu katika historia ya mbio za Marathon katika Michezo ya Olimpiki kwa upande wa wanawake.Sumgong alimaliza  mbio hizo kwa muda wa saa 2 dakika 24 na sekunde 04, akifuatwa na Eunice Jepkirui Kirwa raia wa Bahrain, ambaye alibadilisha uraia wake kutoka nchini Kenya mwaka 2013.Tunajadili hili na mengine mengi yanayoendelea nchini Brazil.