Olimpiki 2016: Jemima Jelagat Sumgong ashindia medali ya dhahabu

Jemima Jelagat Sumgong, mshindi wa mbio za Marathon katika mashindano ya  Olimpiki, Agosti 14, 2016 Rio de Janeiro.
Jemima Jelagat Sumgong, mshindi wa mbio za Marathon katika mashindano ya Olimpiki, Agosti 14, 2016 Rio de Janeiro. AFP

Jemima Jelagat Sumgong, raia wa Kenya, mwenye umri wa miaka 31, ameipatishia nchi yake ushindi wa kwanza katika mashindano ya wanawake ya marathon, ambaye amekimbia muda wa saa 2:24 na sekunde 04, Jumapili hii Agosti 14 katika mji wa Rio de Janeiro, nchini Brazil.

Matangazo ya kibiashara

Sumgong, mshindi wa mashindano ya Marathon yaliyofanyika mwaka huu katika mji wa London, nchni Uingereza, amemshinda Eunice Kirwa Jepkiruiraia wa Baharain, mwenye asili ya Kenya, ambaye amekimbia muda wa saa 2h:24 na sekunde 13). Na Mare Dibaba, raia wa Ethiopia amekimbia saa 2:24 na sekunde 30).

Wakimbiaji hao wamekimbia kilomita 42.195, licha ya baadhi ya waandamanaji kujaribu kuvuruga hatua ya mwisho ya mbio hizo.

Sumgong ataendelea kukumbukwa katika siku zijazo kwa kuwa Mkenya wa kwanza kupata medali ya dhahabu katika mbio hizi za Kilomita 42 katika michezo hii ya Olimpiki inayoendelea nchini Brazil.

Wakenya wengine kama Catherine Ndereba na Prisca Jeptoo, katika miaka iliyopita wamekuwa wakijaribu kupata medali ya dhahabu bila mafanikio.