BRAZIL-MICHEZO YA OLIMPIKI

Usain Bolt bado mfalme wa mita 100 katika mashindano ya Olimpiki 2016

Mwanariadha kutioka Jamaica Usain Bolt baada ya ushindi wake katika mbio za mita 100 katika mashindano ya Michezo ya Olimpiki 2016.
Mwanariadha kutioka Jamaica Usain Bolt baada ya ushindi wake katika mbio za mita 100 katika mashindano ya Michezo ya Olimpiki 2016. REUTERS/Dylan Martinez

Usain Bolt alishinda kwa mara ya tatu mfululizo medali ya dhahabu katika mbio za mita 100 katika Michezo ya Olimpiki Jumapili hii Agosti 14 katika mji wa Rio de Janeiro. Mwanariadha huyo kutoka Jamaica amemshinda Mmarekani Justin Gatlin na Andre Grasse kutoka Canada katika fainali ya Michezo ya Olimpiki 2016 kwa muda wa sekunde 9. 81.

Matangazo ya kibiashara

Ushindi huo unampa Usain Bolt hatua kubwa katika harakati zake katika Riadha.

Haijawahi kutokea katika historia ya riadha na inaweza tu kuwa kazi ya mwanariadha mkuu wa wakati wote: Usain Bolt. Jumapili hii Agosti 14, 2016 katika mji wa Rio de Janeiro, raia huyo kutoka Jamaica kwa mara ya tatu mfululizo amekua bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita 100.

Mbele yake, hakuna mtu aliyewahi kushinda mara tatu kwenye umbali wa michezo hii katika mashindano ya Michezo ya Olimpiki. muda wa sekunde 9.81 ulitosha kwa Usain Bolt kukamilisha ushindi wake mpya katika fainali ya michezo ya Olimpiki 2016.

Usain Bolt alimbwaga Mmarekani Justin Gatlin (9''89) na Andre Grasse (9''91) kutoka Canada, licha ya kuanza kwa misukosuko. Itakumbuka kwamba Akani Simbine kutoka Afrika Kusini amechukua nafasi ya 5 baada ya kukikbimbia muda wa sekunde 9.94) na nafasi ya 6 ilichukuliwa na Ben Youssef Meite ambaye alikimbia muda wa sekunde 9.96.

Na sasa mita 200

Bolt, tayari alipata taji mwaka 2008 katika mashindano ya mjini Beijing na mwaka 2012 katika mashindano mjini London, kwa mara nyingine tena alikua bingwa bora katika mashindano ya mjini Gatlin, baada ya kusimamishwa kwa miaka kadhaa kutokana na madawa ya kusisimu misuli. Usain Bolt mwenye umri wa miaka 29 sasa atajaribu kuongeza medali mbili za dhahabu kwa saba ambazo tayari alishinda katika mashindano ya michezo ya Olimpiki.

Usain Bolt atashiriki mbio za mita 200 kati ya 16 na 18 Agosti.