RIO OLIMPIKI 2016

Bolt aibuka kinara mita 200, asubiri mbio za mita 4x100, Marekani yaomba radhi

Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt, ambaye amejinyakulia medali ya pili ya dhahabu kwenye michezo ya Rio.
Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt, ambaye amejinyakulia medali ya pili ya dhahabu kwenye michezo ya Rio. REUTERS/Lucy Nicholson

Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt, amefanikiwa kunyakua medali ya pili ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio, Brazil baada ya kushinda kwenye mbio za mita 200, ikiwa ni medali yake ya 8 kuinyakua kwenye michezo ya Olimpiki.

Matangazo ya kibiashara

Bolt alikimbia kwa muda wa sekunde 19.78 akimpita Mcanada Andre de Grasse na Mfaransa Christophe Lemaitre.

Muingereza Adam Gemili alimaliza kwenye muda sawa na Mfaransa Lemaitre, lakini alishindwa kupata medali yake ya kwanza baada ya mfumo wa picha kutumika kuamua mshindi.

Botl mwenye umri wa miaka 29, tayari ameshinda mita 100 kwenye michezo ya mwaka huu na anatarajiwa kukimbia kwenye mbio za mita 4x400 za kupokezana vijiti usiku wa kuamkia Jumamosi.

Katika hatua nyingine kamati ya Olimpiki ya Marekani imeomba radhi kwa kile ilichosema tabia isiyokubalika ya waogeleaji wake wa nne ambao walidanganya kwa kutoa taarifa za uongo wakidai waliporwa mali zao na majambazi.

Polis iliwahoji waogeleaji hao wa tatu wa Marekani, ambao baadae walidai kuwa hawakuwa wahanga wa tukio la uporaji kama walivyoripoti awali.

Wanamichezo wawili kati yao, Gunnar Bentz na Jack Conger waliruhusiwa kusafiri kurudi kwao Alhamisi ya wiki hii.

Mchezaji Ryan Lochte tayari ameondoka Rio na James Feigen bado yuko Brazil.

Kwenye masumbwi, kiongozi mkuu anayesimamia mchezo wa masumbwi kwenye michezo ya Rio, amebadilishwa kazi baada ya kukosolewa kutokana na uamuzi wa majaji na marefa waliosimamia baadhi ya mapambano.

Shirikisho la kimataifa la mchezo wa masumbwi, Aiba, limesema kuwa mkurugenzi Karim Bouzidi atapewa majukumu mengine ndani ya taasisi hiyo na nafasi yake itazibwa na mtu mwingine.