CAF-MICHEZO

ZESCO United kumenyana na Mamelodi Sundowns

Wachezaji wa klabu ya E.S Setif ya Algeria wakiwa hawaamini kinachotokea uwanjani baada ya mashabiki wao kufanya vurugu kwenye mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, mchezo wa klabu bingwa Afrika, Juni 18, 2016
Wachezaji wa klabu ya E.S Setif ya Algeria wakiwa hawaamini kinachotokea uwanjani baada ya mashabiki wao kufanya vurugu kwenye mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, mchezo wa klabu bingwa Afrika, Juni 18, 2016 DR

Klabu ya soka ya ZESCO United kutoka Zambia itachuana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Zesco united ilimaliza ya pili katika michuano ya hatua ya makundi baada ya kutamatisha mechi yake ya mwisho jana kwa kutoka sare ya bao 1 kwa 1 na Wydad Casabalanca ya Morocoo mjini Ndola.

Nayo Wydad Casablanca iliyomaliza ya kwanza katika kundi hilo itachuana na Zamalek ya Misri katika hatua hiyo ya nusu fainali.

Mechi hizi zitachezwa nyumbani na ugenini mwezi ujao wa Septemba.

Ni wazi kuwa vlabu vyote vilivyofika katika hatua hii ni kutoka Kusini na Kaskazini mwa Afrika.