SOKA-UEFA

Michuano ya UEFA hatua ya makundi kuanza kurindima

Michuano ya soka hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya UEFA, msimu wa mwaka 2016-17  inaanza kutifua vumbi katika mataifa mbalimbali barani Ulaya Jumanne usiku.

Wafanyakazi wa Uefa wakitandaza uwanjani moja ya bango la shirikisho la mpira Ulaya
Wafanyakazi wa Uefa wakitandaza uwanjani moja ya bango la shirikisho la mpira Ulaya REUTERS/Regis Duvignau Livepic
Matangazo ya kibiashara

Nchini Ufaransa, Paris Saint-Germain ambayo ipo  katika kundi A, itaikaribisha Arsenal ya Uingereza jijini Paris kuanzia saa saa tatu na dakika 45 usiku saa za Afrika Mashariki.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anatarajiwa kumtumia mchezaji mpya Shkodran Mustafi aliyesajiliwa msimu huu huku Aaron Ramsey, akikosa mchuano huu kwa sababu ya jeraha.

Kwingineko, Basel ya Uswizi nayo itashuka dimbani kumenyana na Ludogorets Razgrad ya Bulgaria katika mchuano muhimu wa ufunguzi.

Mabingwa wa zamani Barcelona FC ya Uhispania itamenyana na Celtic FC ya Scotland.

Bracelona inakwenda katika mchuano huu wa ufunguzi ikiwategemea wachezaji wake muhimu kama Lionel Messi, Luis Suarez na Andres Iniesta ambao mwishoni mwa wiki iliyopita, walipumzishwa kupisha mchuano huu wa ufunguzi.

Wawakilishi wengine wa Uingereza Manchester City watakuwa nyumbani katika uwanja wa Etihad kuchuana na Borrusia Monchengladbach ya Ujerumani.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola, anatarajiwa kumtumia mchezaji mpya Ilkay Gundogan raia wa Uhsipania ambaye amekuwa akisumbuliwa na jeraha na kumweka nje ya kikosi cha City.

Sergio Aguero mshambuliaji mwenye uzoefu akitarajiwa kuanza katika mchuano huu muhimu wa ufunguzi.

Ratiba nyingine siku ya Jumanne Septemba 13 2016

 • Dymano Kyiev vs Napoli
 • Bnefica vs Besiktas
 • Bayern Munich vs Rostov
 • PSV vs Atletico Madrid

Mabingwa watetezi Real Madrid ya Uhispania siku ya Jumatano watakuwa nyumbani dhidi ya Sporting Lisbon ya Ureno.

Ratiba ya Jumatano Septemba 14 2016

 • Bayern Leverkusen vs CSKA Moscow
 • Tottenham Hotspurs vs Monaco
 • Legia Warszawa vs Borussia Dortmund
 • Club Brugge vs Leicester City
 • Porto vs Kobenhavn
 • Olympique Lyonnais vs Dinamo Zagreb
 • Juventus vs Sevilla