SOKA-UEFA

Real Madrid kuanza kutetea taji lake dhidi ya Sporting Lisbon nyumbani

Kikosi cha Real Madrid kikijiandaa dhidi ya Sporting Lisbon
Kikosi cha Real Madrid kikijiandaa dhidi ya Sporting Lisbon Uefa

Mabingwa watetezi wa taji la soka la klabu bingwa barani Ulaya UEFA, Real Madrid ya Uhispania wanashuka dimbani kumenyana na Sporting Lisbon ya Ureno katika mchuano wake wa kwanza wa hatua ya makundi.

Matangazo ya kibiashara

Huu ni mchuano unaoleta kumbukumbu kwa mshambuliaji wa klabu hiyo Christiano Ronaldo atakayecheza mechi yake ya 132 katika michuano hii dhidi ya klabu yake ya zamani, aliyoichezea akiwa na miaka 12.

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema anaamini kuwa wapinzani wao watakuja kwa nguvu kutafuta ushindi wa mapema huku Jorge Jesus kocha wa Sporting Lisbon, akidokeza kuwa anakwenda kupambana na kikosi kigumu cha Real Madrid.

Kikosi cha timu zote mbili:-

Real Madrid : Casilla; Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo; Modric, Casemiro, Kroos; Bale, Benzema, Ronaldo

Sporting Lisbon : Rui Patricio; Pereira, Coates, Semedo, Zeegelaar; Silva, Carvalho; Martins, Ruiz, Cesar; Dost

Ratiba nyingine hivi leo:-

 • Bayern Leverkusen vs CSKA Moscow
 • Tottenham Hotspurs vs Monaco
 • Legia Warszawa vs Borussia Dortmund
 • Club Brugge vs Leicester City
 • Porto vs Kobenhavn
 • Olympique Lyonnais vs Dinamo Zagreb
 • Juventus vs Sevilla

Matokeo ya michuano ya Jumanne Septemba 13 2016:-

 • Basel 1-1 Ludogorets
 • PSG 1-1 Arsenal
 • Dymano Kyiev 1-2 Napoli
 • Bnefica 1-1 Besiktas
 • Bayern Munich 5-0 Rostov
 • PSV 0-1 Atletico Madrid