SOKA-CECAFA

Kenya, Uganda, Tanzania na Uganda zafuzu nusu fainali ya michuano ya CECAFA

Tanzania ikimenyana na Ethiopia katika mchuano wa kumaliza hatua ya makundi taji la CECAFA Septemba 15 2016 mjini Jinja
Tanzania ikimenyana na Ethiopia katika mchuano wa kumaliza hatua ya makundi taji la CECAFA Septemba 15 2016 mjini Jinja Kawowo Sport

Timu ya taifa ya soka ya Kenya itamenyana na Ethiopia katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la CECAFA kwa upande wa wanawake, katika michuano inayoendelea katika taasisi ya kukuza soka ya Njeru mjini Jinja nchini Uganda.

Matangazo ya kibiashara

Katika mchuano mwingine, wenyeji Uganda watamenyana na Tanzania bara.

Michuano hii yote utapigwa siku ya Jumapili, huku fainali ikichezwa siku ya Jumanne wiki ijayo.

Siku ya Jumamosi ni siku ya mapumziko.

Harambee Starlets ya Kenya ilifuzu baada ya kushinda mechi zake zote za kundi A, na kutofungwa bao lolote.

Hivi ndivyo matokeo yalivyokuwa:

  • Kenya 4-0 Uganda
  • Kenya 4-0 Burundi
  • Kenya 11-0 Zanzibar

Uganda nayo ilimaliza ya pili katika kundi hili la A.

  • Uganda 0-1 Kenya
  • Uganda 9-0 Zanzibar
  • Uganda 1-0 Burundi

Kilimanjaro Queens ya Tanzania bara nayo ilifuzu huku mchuano wake wa mwisho dhidi ya Lucy ya Ethiopia ikimalizika kwa sare ya kutofungana.

Matokeo ya Tanzania katika michuano hii:-

  • Tanzania 3-2 Rwanda
  • Tanzania 0-0 Ethiopia

Ethiopia nayo ilifuzu baada ya kumaliza ya pili katika kundi B kwa alama nne baada ya kuifunga Rwanda mabao 3-2.