CECAFA-WANAWAKE

Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania yatwaa taji la Cecafa, yaweka historia

Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake wa Tanzania, wakishangilia moja ya magoli waliyofunga kwenye michuano ya mwaka huu ya Cecafa iliyofanyika nchini Uganda
Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake wa Tanzania, wakishangilia moja ya magoli waliyofunga kwenye michuano ya mwaka huu ya Cecafa iliyofanyika nchini Uganda fufa.com

Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Taifa Queens imekuwa timu ya kwanza kutwaa taji la michuano ya soka inayosimamiwa na baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Katim CECAFA.

Matangazo ya kibiashara

Michuano ya mwaka huu ambayo ilikuwa ni ya kwanza kufanyika, imeshuhudia wawakilishi wa Kenya, Harambee Starlets ambao watauwakilisha ukanda wa Afrika Mashariki kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika nchini Cameroon kuanzia mwezi November mwaka huu, walicheza mchezo wa fainali na Tanzania.

Harambee Starlets ambayo ilikuwa iknatumia pia sehemu ya michuano hiik kujipima kabla ya kuelekea kule Afrika Kusini, ilianza vema safari yake hadi kufika hatua ya fainali, ambapo kikosi hicho kimeonesha kuimarika.

Kwenye mchezo huo, timu ya taifa ya Tanzania bara ya wanawake ilifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1, huku bao la ushindi la Tanzania likifungwa katika dakika za lala salama.

Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Njeru jijini Kampala, ulishuhudia fataki la winga wa Tanzania, Mwanahamisi Omar likiipa uongozi timu yake hadi dakika 45 za mwanzo zilipokamilika.

Harambee Starlets ilirejea kwa nguvu kwenye kipindi cha pili cha mchezo huo na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kabla ya Tanzania kupata bao la 2 na la ushindi lililofungwa kwenye dakika za lala salama.

Matokeo haya yameifanya timu ya wanawake ya Tanzania, kuwa mabingwa wapya kabisa wa michuano ya mwaka huu kwa upande wa wanawake na kuweka historia kwenye michuano hii ya kwanza ya wanawake inayosimamiwa na CECAFA.

Kwenye mchezo wa kusaka mshindi wa tatu timu ya taifa ya Ethiopia ilikuwa ikipepetana na timu ya taifa ya Uganda ambao walikuwa wenyeji wa michuano ya mwaka huu, katika mchezo ulioshuhudia, Ethiopia wakichomoza na ushindi mnono wa mabao 4-1, ushindi uliowafanya wachukue nafasi ya tatu.

Washabiki wa Soka nchini Uganda na kwenye ukanda wa Afrika Mashariki waliozungumza na idhaa hii, wameeleza kuridhishwa na namna michuano ya mwaka huu imeandaliwa lakini wakatoa wito kwa CECAFA kusaka wadhamini zaidi na kuongeza timu washiriki.