CCL-CL-CAF

Zamalek, Mamelod Sundowns kucheza fainali ya klabu bingwa barani Afrika

Wachezaji wa klabu ya Mamelod Sundowns wakiwapungia mkono mashabiki baada ya kufuzu fainali kwa kuwaondoa Zesco United ya Zambia
Wachezaji wa klabu ya Mamelod Sundowns wakiwapungia mkono mashabiki baada ya kufuzu fainali kwa kuwaondoa Zesco United ya Zambia Goal.com

Klabu ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini hatimaye imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza hatuaj ya fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika, baada ya kuchomoza na ushindi wa mabo 2-0 dhidi ya Zesco United ya Zambia kwenye mchezo wa marudiano uliopigwa usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili.

Matangazo ya kibiashara

Kwa ushindi huo sasa, Mamelod watacheza hatua ya fainali dhidi ya waliowahi kuwa mabingwa mara kadhaa wa taji hili, klabu ya Zamalek ya Misri, ambayo usiku wa kuamkia Jumapili ya September 25, licha ya kukubali kichapo cha mabao 5-2, bado ilifuzu kwa faida ya mabao ya kufunga.

Mamelod Sundowns ambayo ilikuwa nyumbani, ilipoteza mchezo wa awali mjini Ndola Zambia kwa jumla ya mabao 2-1, na iliwalazimu kushinda mchezo wa Jumamosi, ili wafuzu kucheza hatua ya fainali, ndoto ambayo waliitimiza.

Wenyeji Sundowns ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mchezaji wake mahiri Anthony Laffor kabla ya kupigilia msumari wa mwisho katika dakika za lala salama na kuondoka na ushindi wa mabo 2-0, ushindik uliotosha kuivusha kucheza hatua ya fainali.

Sundowns ambayo awali ilikuwa imetolewa kwenye hatua ya makundi, ilirejeshwa baada ya klabu ya Esparance kutolewa kwenye michuano hiyo kutokana na mashabiki wake kufanya vurugu uwanjani.

Matokeo haya hata kama yangekuwa kwa sare ya mabao 2-2, bado Sundowns ingesonga mbele kucheza fainali kwa faida ya bao la ugenini.

Mchezo uliowaduwaza wengi ulikuwa ni ule wa kati ya Zamalek ya Misri ambao walikuwa ugeninik kucheza na Wydad Casablanca, katika mchezo ambao almanusura klabuj hiyo ishindwe kusonga mbele kama si faida ya mabo mawili waliyoyafunga ugenini.

Wachezaji wa timu ya Zamalek wakipongezana baada ya kupata bao kwenye mchezo dhidi ya Wydad na kufuzu kucheza hatua ya fainali.
Wachezaji wa timu ya Zamalek wakipongezana baada ya kupata bao kwenye mchezo dhidi ya Wydad na kufuzu kucheza hatua ya fainali. Goal.com

Zamalek ambayo kwenye mchezo wa awali ilishinda kwa mabao 4-0, ilikuwa inahiyajik sare tu ili kusonga mbele, lakini kipigo cha kushangaza cha mabao 5-2 almanusura kizime ndoto yao ya kucheza hatua ya fainali ambapo mara ya mwisho ilicheza fainali hizo miaka 14 iliyopita.

Zamalek imefuzu kucheza fainali kwa faida ya mabo mengi ya kufunga yakiwemo yale ya ugenini, ambapo imefuzu kwa jumla ya mabao 6-5.

Wydad ambayol ilimfuta kazi kocha wake mkuu, John Toschack Jumatatu ya wiki iliyopita, ilikuwa inajaribu kuwa timu ya kwanza kugeuza matokeo ya 4-0 na kufuzu kucheza fainali.

Mliberia William Jebor aliifungia timu mabao mawili na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko kwa mabao 3-1, ambapo bao la tatu lilifungwa na Ismail El Haddad, huku lile bao la Zamalek likifungwa na Basem Morsi.

Dakika 10 za lala salama zilikuwa mwiba kwa Wydad ambayo iliruhusu Zamalek kupata bao la pili ambalo lilitosha kufanya mchezo huo kumalizika kwa jumla ya mabao 5-2, na hivyo Zamalek kufuzu kwa idadi kubwa ya mabao.

Fainali ya mwaka huu itapigwa October 14.

Bingwa wa fainali hii ataliwakilisha bara la Afrika kwenye michuano ya klabu bingwa ya Dunia inayotarajiwa kupigwa mwezi December mwaka huu.