SOKA-UEFA

Borrusia Dortmund kuwakaribisha Real Madrid katika mechi muhimu ya UEFA

Michuano ya mzunguko wa pili hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya UEFA, inapigwa Jumanne usiku katika viwanja mbalimbali katika bara hilo.

Wachezaji wa klabu ya Borrusia Dortmund wakifanya mazoezi kabla ya mchuano wa Septemba 27 2016
Wachezaji wa klabu ya Borrusia Dortmund wakifanya mazoezi kabla ya mchuano wa Septemba 27 2016 uefa
Matangazo ya kibiashara

Mabingwa watetezi Real Madrid ya Uhispania na Borrusia Dortmund ambazo zipo katika kundi moja la F, zinakutana katika mchuano  muhimu baada ya kushinda mechi za ufunguzi.

Katika michuano minne iliyopita, Dortmund wameishinda Madrid, rekodi ambayo wanatarajiwa kuiendeleza katika mchuano wa Jumanne.

Kocha wa Borrusia Dortmund Thomas Tuchel, amesema anatambua Madrid ina kikosi kizuri cha wachezaji kama Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na Karim Benzema na hivyo chochote kinaweza kutokea.

Hata hivyo, kocha wa Madrid Zinédine Zidane, kuelekea katika mchuano huu, amesema kuwa anatambua kuwa mchuano huu utakuwa mgumu na amewaambia wachezaji wake wajaribu kutafuta mabao ya mapema.

Ratiba ya mechi zingine za leo:-

  • CSKA Moscow vs Tottenham Hotspurs
  • Leicester vs FC Porto
  • Monaco vs Bayer Leverkusen
  • Sporting vs Legia
  • Sevilla vs Lyon