Jukwaa la Michezo

Watani wa jadi nchini Tanzania SImba na Yanga watoshana nguvu

Sauti 23:55
Simba FC ikimenyana na Yanga FC katika mchuano muhimu wa ligi kuu nchini Tanzania
Simba FC ikimenyana na Yanga FC katika mchuano muhimu wa ligi kuu nchini Tanzania shaffihdauda.co.tz

Watani wa jadi katika mchezo wa soka nchini Tanzania Simba FC na Yanga FC, wametoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mchuano muhimu wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Mchuano huo ulikumbwa na vurugu na mashabiki wa Simba kungo'a viti uwanjani baada ya mwamuzi mchezo huo kuipa Yanga bao kipindi cha kwanza, baada ya mfungaji Ammis Tambwe kudaiwa kuunawa kabla ya kuufunga.