CAMEROON-RIGOBERT SONG

Cameroon: Rigobert Song katika hali ya mahututi

Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya soka ya Cameroon, Rigobert Song.
Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya soka ya Cameroon, Rigobert Song. Reuters

Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon Rigobert Song, amelazwa hospitalini na anatazamiwa kusafirishwa barani Ulaya, baada ya kupatwa maradhi ya kiharusi Jumapili, Oktoba 2 mjini Yaounde. Mchezaji huyo nduli amekua katika hali ya mahututi Jumatatu Asubuhi, kwa mujibu wa redio ya serikali ya Cameroon.

Matangazo ya kibiashara

Jumapili, Oktoba 2, Rigobert Song alipatwa maradhi ya kiharusi. mchezaji wa zamani wa Metz na Lens alikuwa Jumatatu hii asubuhi "katika hali ya mahututi", redio ya taifa ya Cameroon imearifu. Serikali inapanga kumpatishia huduma za kimatibabu barani Ulaya, na anatazamiwa kusafirishwa katika ndege maalumu "yenye dawa" kwa mujibu wa redio ya serikali ya Cameroon (CRTV). Nahodha wa timu ya soka taifa ya Cameroon ambaye kwa sasa ni kocha wa Timu ya Cameroon ya daraja la kwanza amelazwa katika kituo cha Dharura mjini Yaounde.

Rekodi ya ushiriki katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika

"Nakutakia ahueni na upone haraka kaka yangu," Samuel Eto'o amesema kwenye ukurasa wake wa Facebook. Itafahamika kwamba Samuel Eto'o alikuamchezaji mwenza wa Songo katika timu ya taifa ya soka ya Cameroon. Rais wa Cameroon, Paul Biya, ameomba kufanyika kwa lolote lile ili kunusuru maisha ya beki wa zamani wa timu ya taifa ya soka ya Cameroon.

Nahodha wa Simba wa Nyika, ambaye anajulikana kwa jina maarufu "Magnan" ikimaanisha tajiri, anashikilia rekodi ya ushiriki katika michezio ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mashindano 8 na mechi 36. Rigobert Song ameshirikishwa katika mara 137 na pia alicheza fainali nne za Kombe la Dunia (1994, 1998, 2002, 2010). Rigobert Song alistaafu kimataifa mwaka 2010. Yeye pamoja na Samuel Eto'o walianza kuchezeamichuano ya Kombe la Dunia wakiwa na umri mdogo.

Mbali na Ufaransa, Rigobert Song alicheza hasa nchini Uingereza, katika klabu ya Liverpool, na Uturuki katika klabu mbili: Galatasaray na Trabzonspor, ambapo alishinda mataji mawili Ligi kuu ya Uturuki.