SUPER EAGLE-SOKA

Super Eagles yajiandalia Kombe la Dunia 2018

Mechi ya kufuzu kati ya Nigeria na Misri kwa michuano ya AFCON 2017, mwezi Machi 2016, mjini Kaduna.
Mechi ya kufuzu kati ya Nigeria na Misri kwa michuano ya AFCON 2017, mwezi Machi 2016, mjini Kaduna. AFP

Kutokana na ukosefu wa fedha, timu ya taifa ya soka ya Nigeria itawasili nchini Zambia masaa 22 tu kabla ya mechi yake dhidi ya Zambia, katika michuano ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018.

Matangazo ya kibiashara

Safari ya Super Eagles imecheleweshwa kwa matatizo ya kifedha, Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) limejieleza mbele ya Kamati inayohusika na michezo katika baraza la Seneti la Nigeria.

Wachezaji watmeondoka Nigeria Alhamisi hii na watawasili nchini Zambia Jumamosi mchana na kumenyana na Chipolopolo Jumapili, mwishoni mwa juma hili.

Timu ya taiafa ya soka ya Nigeria watakua watakua na mazoezi kabla ya mchuano kati yake na Chipolopolo.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa shirikisho la soka la Nigeria (NFF), Amaju Pinnick, shirikisho la soka la Nigeria lilipata tatizo la kulipa nauli ya ndege na malazi kwa wachezaji.

NFF imewaomba wachezaji waishio Ulaya kununua nauli za ndege kwa minajili ya kujiunga na wachezaji wa timu yao ya taifa mjini Abuja, mji mkuu wa Nigeria, Pinnick amewalezea maseneta wanaohusika na masuala ya michezo.

Nigeria inakabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi.

Uchumi wake unadorora tangu mwishoni mwa mwezi Agosti, ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu miaka 10 iliyopita.