TENESI

Murray atinga nusu fainali michuano ya China Open

Mscotland Andy Murray.
Mscotland Andy Murray. Reuters/Kevin Lamarque

Mchezaji tenesi nambari mbili kwa ubora wa mchezo huo duniani, Andt Murraym amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya China Open, baada ya kumfunga Muingereza mwenzake Kyle Edmund kwa seti 7-6 na 6-2.

Matangazo ya kibiashara

Murray mwenye umri wa miaka 29 hivi sasa, alijikuta akipata upinzani mkali kwenye seti ya kwanza na kulazimika kucheza zaidi kupata mshindi wa jumla baada ya kulingana alama, lakini akajikuta akifanya vizuri kwenye seti ya pili.

Lakini Edmund ambaye sasa atapanda na kuingia kwenye orodha ya 50 bora ya wachezaji wa mchezo huo baada ya kumfunga Muhispania Roberto Bautista Agut kutinga hatua ya nane bora, lakini akapoteza kwa seti tatu na Andy Murray.

Murray sasa atacheza na Muhispania mwingine David Ferrer kwenye hatua ya nusu fainali.

Ilikuwa ni wakati mgumu kwa Edmund ambaye alimbana vilivyo Murray katika seti ya kwanza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye mwezi February aliorodheshwa kwenye wachezaji 100 wa mchezo huo duniani, sasa atajikuta akipaa hadi kuingia kwenye orodha ya 50 bora.

Murray amepoteza mchezo mmoja tu katika michezo ya kimataifa anapokutana na waingereza wenzake, ambapo mwaka 2006 alifungwa kwa seti mbili bila na Tim Henman jijini Bangkok. Hii ni mara ya pili ndani ya mwaka huu kwa Murray kumfunga Edmund, kwani alimfunga wakati alipokutana kwenye mashindano ya Aegon.

Katika mechi nyingine mchezaji Rafael Nadal anacheza na Mbulgaria Grigor Dimitrov kwenye hatua ya robo fainali wakati Milos Raonic akicheza na Muhispania Pablo Carreno Busta kwenye robo fainali nyingine.