KOMBE LA DUNIA 2018-SOKA

Kombe la Dunia 2018: Misri yaishinda Congo ugenini

Timu ya taifa ya soka ya Misri wamewashinda Congo mjini Brazzaville mabao 2-1. Misri wanaongoza katika kundi E baada ya mshindani wake mkuu katika kundi hili, Ghana, waliotoka sare ya kufungana na Uganda 1-1. Wachezaji nyota wa Misri Mohamed Salah na Abdalla El Said ndio waliipatishia ushindi timu yao.

Mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah akisheherekea bao lake dhidi ya Botswana.
Mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah akisheherekea bao lake dhidi ya Botswana. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Baada ya matokeo yaliyowashangaza wengi katika mechi iliyozikutanisha timu ya taifa ya soka ya Ghana na Uganda Ijumaa Oktoba 7, Misri imejikuta ikiongoza katika kundi E, baada ya kuwafunga Congo, mjini Brazzaville Jumapili hii Oktoba 9.

Congo ndio walianza kuliona lango la Misri katika dakika ya 24 ya mchezo kupitia mchezaji Férébory Doré, baada ya kupewa pasi nzuri na Thievy Bifouma, mchezaji wa klabu ya Angers (daraja la kwanza, nchini Ufaransa), kipa wa Misri Essam El-Hadary alijikuta mpira ukichezea wavuni.

Mbali na kushambuliwa, Misri ilikuja juu kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika na kufunga bao la kwanza, dakika nne kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika kupitia mchezaji Mohamed Salah, ambaye alifungwa bao hilo kwa kichwa, baada ya kupokea pasi kutoka kwa Abdul Shafy katika dakika ya 41.

Bao la pili la Misri lilifungwa baada ya Mohamed Salah wa klabu ya AS Roma (ligi A nchini Italia) kutoa pasi nzuri kwa Abdalla El Said, ambapo kipa wa Mashetani Mekundu, Gildas Mouyabi, alikataa tamaa.

Mechi nyingine iliyopigwa leo ni kati ya Tunisia na Guinea. Tunisia imewashinda nyumbani Guinea mabao 2-0.

Itakumbukwa kwamba Chui wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo waliinyeshea mvua ya magoli Libya, Ambapo hadi dakika ya mwisho ya mchezo Libya ilijikuta ikifungwa mabao 4-0. Mechi kati ya timu hizi mbili ilipigwa Jumamosi jioni katika uwanja wa Martyrs.