TIGER WOODS-PGA

Tiger Woods ahairisha kwa muda kurejea uwanjani, sasa kurudi mwezi December

Mchezaji Tiger Woods katika picha ambaye ameahirisha kurejea kwenye mashindano na alikuwa kama nahodha msaidizi wa timu ya Marekani wakati wa muchuano ya Ryders Cup.
Mchezaji Tiger Woods katika picha ambaye ameahirisha kurejea kwenye mashindano na alikuwa kama nahodha msaidizi wa timu ya Marekani wakati wa muchuano ya Ryders Cup. John David Mercer-USA TODAY Sports

Mchezaji gofu maarufu duniani, Tiger Woods, ameahirisha kushiriki kwenye mashindano ya mchezo huo ya Safeway Open, kwa kile anachosema kuwa mchezo wake bado haujarejea kwenye kiwango na pia afya yake kuimarika.

Matangazo ya kibiashara

Woods ambaye ni bingwa mara 14 wa mataji makubwa PGA, hatashiriki mashindano hayo, ambayo yangeshuhudia akirejea kwenye ushindani baada ya kuwa nje ta mchezo huo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Woods mwenye umri wa miaka 40 hivi sasa, mara ya mwisho alishindana mwaka 2015, ambapo wakati huo tayari alishakuwa amefanyiwa upasuaji mdogo wa mgongo kwa zaidi ya mara mbili.

Mchezaji huyo sasa amepanga kurejea kwenye mashindano mwanzoni mwa mwezi December mwaka huu, wakati wa mashindano ya Hero World Challenge, ambayo huandaliwa kwenye visiwa vya Bahama.

Mchezaji huyu ambaye aliwahi pia kushika nafasi ya kwanza kwa ubora wa mchezo huo duniani, na sasa anashika nafasi ya 786, amesema amefikia uamuzi huu baada ya tafakuri ya kina na kutafuta kile ambacho anapenda kukifanya zaidi.

Mwezi September mwaka huu Toger Woods alitangaza kuwa angerejea kwenye mashindano ya safeway Open kabla ya kushiriki mashindano ya Turkish Airlines Open mwezi November mwaka huu.

Woods amesema kuwa “afya yangu ni njema na najisikia niko imara, lakini kimchezo siko tayari na wala kiwango changu hakipo napotaka kiwe, nakaribia na sitaacha mpaka nifike nakotaka.” alisema mchezaji huyo.

Woods alikuwa naibu nahodha wa timu ya taifa ya Marekani ya mchezo wa Gofu ambayo ilishinda taji la Ryder mwezi huu.

Mchezaji huyu hakushiriki kwenye mashindano yoyote ya msimu wa mwaka 2015 na 2016 kutokana na kuendelea kuuguza majeraha ambapo wakati huo alikuwa amecheza kwenye mashindano 11 peke yake misimu iliyopita.