AFCON 2017-SOKA

AFCON 2017: makundi hatimaye yajulikana

Tuzo ya mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika.
Tuzo ya mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Droo ya Kombe la Mataifa ya Afrika imefanyika Jumatano hii tarehe 19 Oktoba katika mji wa Libreville, nchini Gabon. Gabon, ambayo itakua mwenyeji wa michuano hii itakuwa kibarua kigumu kwa kukabiliana na Burkina Faso, Cameroon na Guinea-Bissau katika michuano hii ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2017).

Matangazo ya kibiashara

Mechi ya ufunguzi itakua kati ya Gabon, mwenyeji na Guinea-Bissau Januari 14, 2017. Mechi hii ya ufunguzi itakuwa muhimu kwani itakuwa mara kwanza katika historia ya Guinea-Bissau kushiriki michuano hii ya kimataifa. Ni vigumu kufanya vizuri ikiwa ndio bado unashiriki michuano yenyewe . Kwa upande wa Gabon, itakua vema kuanza kupata ushindi mapemakwa timu hii ambayo ni changa katika michuano hii ya kimataifa

Kundi A inaundwa na Gabon, Burkina Faso, Cameroon, Guinea-Bissau. Mechi zitachezwa katika mji wa Libreville.

Kundi B inaundwa na Algeria, Tunisia, Senegal, Zimbabwe. Mechi zitapigwa katika mji wa Franceville.

Kundi C linaundwa na Cote d'Ivoire, DR Congo, Morocco, Togo. Mechi zitapigwa katika mji wa Oyem.

Misri hautakuwa alishinda nchi

Kundi D linaundwa na Ghana, Mali, Misri, Uganda. Mechi zitachezwa katika mji wa Port-Gentil.

Michuano ya 31 ya Kombe la Mataifa ya Afrika itachezwa kuanzia Januari 14 hadi Februari 5, 2017 nchini Gabon.