MCHEZO-RAGA

Wachezaji wa raga wafutiwa tuhuma ya kutumia madawa ya kusisimua mwili

Dan Carter katika fainali ya Kombe la Ulaya mchezo wa raga, mjini Lyon Mei 2016.
Dan Carter katika fainali ya Kombe la Ulaya mchezo wa raga, mjini Lyon Mei 2016. Getty Images

Dan Carter, mchezaji wa Racing 92, amefutiwa tuhuma ya kutumia dawa ya kusisimua mwili aina ya corticosteroids.Tume inayopambana dhidi ya utumiaji wa madawa ya kusisimua mwili ya Shirikisho la Mchezo wa Raga la Ufaransa (FFR) limefuta hatia iliyokua ikimkabilia mchezaji maarufu wa raga kutoka New Zealand.

Matangazo ya kibiashara

Bingwa wa dunia mara mbili amesema kuridhishwa baada ya kutangazwa uamuzi huo Jumanne wiki hii: "Sishangai na uamuzi wa FFR kusema kwamba sijafanya chochote kibaya."

"Nina furaha sana na kwa sasa ninajiandaa kuendelea na mchezo wangu wa raga," amesema Dan Carter, ambaye alichaguliwa mara tatu mchezaji bora duniani.

Wachezaji wenzake Joe Rokocoko na Juan Imhoff pia wamefutiwa 'tuhuma zote zilizokua zikiwakabili,' kwa mujibu wa timu ya Racing 92.

Wakati wa vipimo baada ya fainali ya michuano ya Ufaransa, ambapo Toulon ilishindwa mwezi Juni (29-21), maafisa wa ukaguzi walisema waliona chembechembe za corticosteroids katika mkojo wa wachezaji hao.