CAF-MAMELODI SUNDOWNS-SOKA

Ligi ya Mabingwa CAF: Mamelodi Sundowns yashinda taji

Jumapili Oktoba 23, klabu ya Afrika Kusini Mamelodi Sundowns ilishinda taji lake la kwanza la Ligi ya Mabingwa ya CAF dhidi ya Zamalek kutoka Misri. Mechi ya marudiano ya fainali hii ilichezwa katika uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria, nchini Misri.

Mamelodi Sundowns mshindi wa kwanza katika historia yake wa taji la Ligi ya Mabingwa la CAF
Mamelodi Sundowns mshindi wa kwanza katika historia yake wa taji la Ligi ya Mabingwa la CAF STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa ilishindwa kwa bao moja kwa nunge, klabu hii ya Afrika Kusini ilitwaa taji kutokana na ushindi wake wa mabao matatu kwa nunge, wakati wa mechi ya awali, mjini Pretoria. Mamelodi Sundowns ilipata nafasi ya kuendelea na michuano hii baada ya kushindwa kwa klabu ya Dr Congo ya AS Vita Club. Mamelodi Sundowns imeshinda taji hili baada ya mtangulizi wake klabu nyingine ya DR Congo TP Mazembe kupata ushindi kama huu.

Zamalek ilitawala mpira katika kipindi cha kwanza cha mchezo bila hata hivyo kufanya vizuri. Kipindi cha kwanza kilimalizika timu hizi mbili zikiwa sare ya kutofungana.

Baada ya kutoka mapumziko, Zamalek alijaribu kuja juu na kufanikiwa kuliona bao la Mamelodi Sundowns katika dakika ya 64, bao lililofungwa na mchezaji Ohawushi. Hadi dakika tisini za mchezo ushindi uliku wa Misri wa Bao moja kwa nunge, lakini bao hili halikutosha ili Zamalek itunukiwe taji, kwani katika mechi ya awali ilifungwa mabao matatu kwa nunge.

Miaka ishirini baada ya Afrika Kusinikufanikiwa katika michuano kama hii, ambapo klabu ya Orlando iliibuka mshindi na kutwaa taji dhidi ya ASEC Mimosas.

Mamelodi itawakilisha Afrika katika katika michuano ya Kombe la Dunia ya vilabu.