MAN UNITED-MORINHO

Mourinho akabiliwa na vikwazo

Shirikisho la Soka la Uingereza limefungua kesi ya kinidhamu dhidi ya meneja wa Manchester United Jose Morinho, kufuatia lugha chafu aliyoitoa akihojiwa kuhusu mwamuzi Taylor.

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho (kushoto) akiwa na mwenzake wa Manchester City, Pep Guardiola (kulia), wakikumbatiana wakati timu zao zilipokutana hivi karibuni.
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho (kushoto) akiwa na mwenzake wa Manchester City, Pep Guardiola (kulia), wakikumbatiana wakati timu zao zilipokutana hivi karibuni. Reuters / Carl Recine Livepic
Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la Soka la Uingereza limemuitisha Jose Mourinho, ambaye atajieleza kuhusu kauli aliyoitoa dhidi ya mwamuzi kabla ya mchuano wa mechi iliyochezwa katika mji wa Liverpool katikati ma mwezi Oktoba.

"Nadhani Bw Taylor ni mwamuzi mzuri sana, lakini pia nadhani kama kuna mtu kwa makusudi anayempa shinikizo hatokua mzuri kama alivyo sasa," Mourinho alisema kabla ya klabu yake kutoka sare ya kutofungana (0-0) na klabu ya Anfield tarehe 17 Oktoba.

Jose Morinho anaweza kusimamishwa kwa mechi kadhaa kama atapatikana na hatia ya 'utovu wa nidhamu' kutokana na matamshi hayo.

Mourinho, arudilia makosa yake ya kinidhamu

Kocha huyo Mreno tayari kuadhibiwa kwa lugha chafu alizozitoa katika miaka ya hivi karibuni.

Jose Mourinho alisimamishwa kwa michezo miwili kwa sababu ya kukosoa marefa mwaka 2015.

Alipokua kocha wa klabu ya Real Madrid mwaka 2011, alipewa adhabu kama hiyo, baada ya visa vyake vichafu.

Alishutumiwa kumuweka kidole chake katika jicho la kocha msaidizi wa FC Barcelona baada ya kushindwa kwa timu yake katika mechi ya marudiano ya Super Cup ya Uhispania.