WTA SINGAPORE

Tenesi: Cibulkova amshinda Kerber na kutwaa taji la WTA nchini Singapore

Mslovakia Dominika Cibulkova amefanikiwa kushinda taji lake la kwanza la michuano ya WTA nchini Singapore, baada ya kumfunga mchezaji bora namba moja kwa mchezo wa tenesi upande wa wanawake, Mjerumani Angelique Kerber kwa matokeo ya seti mbili bila kwa 6-3 na 6-4.

Mslovakia Dominika Cibulkova, akibusu kikombe alichoshinda kwenye michuano ya WTA nchini Singapore, 30 October 2016.
Mslovakia Dominika Cibulkova, akibusu kikombe alichoshinda kwenye michuano ya WTA nchini Singapore, 30 October 2016. REUTERS/Edgar Su
Matangazo ya kibiashara

Cibulkova, aliyemaliza kwenye nafasi ya pili wakati wa michuano ya mwaka 2014 ya Australian Open, alibadili matokeo ya Kerber ikiwa ni wiki moja tu toka alipopoteza mchezo dhidi yake.

Kerber aliingia kwenye fainali hii akipewa nafasi ya kutwaa taji la michuano ya Singapore, hasa baada ya kutwaa taji la michuano ya Australian Open ya mwaka huu.

Hata Kerber mwenye umri wa miaka 28 hivi sasa, alijikuta akishindwa kufua dafu mbele ya Mslovakia Cubulkova, ambaye alirejea mwaka huu kwenye mchezo wa tenesi baada ya kuwa nje kwa kitambo kidogo.

Ushindi huu wa Cubulkova umemfanya arejee kwa kishindo katika mashindano makubwa ya tenesi, ambapo msindi wa taji hili la Billie Jean King, anazawadiwa kitita cha dola za Marekani milioni 2, kitita ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kukishinda kwenye historia ya maisha yake ya tenesi.