FIFA-UINGEREZA

May akosoa uamuzi wa Fifa kukataza wachezaji kuvaa ua maalumu kuwakumbuka waliokufa vitani

Kocha wa Wales, Chris Coleman, akiwa amevaa ua maalumu mfano wa Apple ambao Fifa imekataa wachezaji kuvaa.
Kocha wa Wales, Chris Coleman, akiwa amevaa ua maalumu mfano wa Apple ambao Fifa imekataa wachezaji kuvaa. Reuters / Carl Recine Livepic

Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May amesema kuwa uamuzi wa shirikisho la mpira wa miguu duniani Fifa, kukataa ombi lao la kutaka wachezahu timu ya taifa ya Uingereza na Scotland kuvaa vitambaa maalumu mkononi vyenye  alama mfano wa Apple, ni wa kushtua. 

Matangazo ya kibiashara

Nchi hizi mbili zitakutana kwenye mchezo wa Novemba 11, siku ambayo jumuiya ya nchi zinazounda Uingereza, zitakuwa zinaadhimisha kuumbukumbu ya watu waliouawa wakati wa vita.

Shirikisho la kabumbu Fifa, limesisitiza kuhusu uamuzi wake, ambao kwa mujibu wa kanuni na sheria zake, inakataza mpira wa miguu kuhusishwa na siasa au shughuli za kidini kwenye fulana au vitambaa maalumu.

Waziri mkuu May amesema kuwa, kabla hawajatuambia nini cha kufanya, kwanza wangesafisha nyumba yao ambayo ni chafu," alisema kiongozi huyo.

"Wachezaji wetu wanataka kuwakumbuka na kutoa heshima kwa wale waliouawa kwenye vita na kupigana kwaajili ya nchi yetu, na nadhani ilikuwa sahihi kwa wao kuvaa vitambaa hivyo." alisema May.

Juma hili vyama vya soka vya Uingereza na Scotland, viliandika barua kwa shirikisho la mpira wa miguu Fifa, vikiomba kupewa ruhusa kwa wachezaji wao kuvaa vitambaa maalumu siku hiyo kuwakumbuka wanajeshi na watu waliojitolea kuipigania nchi yao.

Uongozi wa Fifa bado haujatoa taarifa yoyote kujibu au kukanusha matamshi ya waziri mkuu May.