SOKA

Urusi 2018: Safari ya kutafuta tiketi kwa mataifa ya Afrika kuendelea

Mzunguko wa pili wa michuano ya soka hatua za makundi kufuzu katika kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018 baina ya Mataifa ya Afrika zinachezwa mwishoni mwa juma hili katika mataifa mbalimbali.

Nembo ya kombe la dunia mwaka 2018
Nembo ya kombe la dunia mwaka 2018 FIFA
Matangazo ya kibiashara

Mataifa 20 yamewekwa katika makundi matano, kila kundi likiwa na mataifa manne.

Baada ya kumalizika kwa michuano ya hatua ya makundi, mshindi katika kila kundi atafuzu katika fainali hiyo ya kombe la dunia na kuliwakilisha bara la Afrika.

Ratiba ya siku ya Jumamosi Novemba 12 2016

  • Afrika Kusini vs Senegal
  • Uganda vs Congo
  • Cameroon vs Zambia
  • Nigeria vs Algeria
  • Cape verde Island vs Burkina Faso
  • Mali vs Gabon
  • Morocco vs Cote d'Ivoire

Ratiba ya siku ya Jumapili Novemba 13 2016

  • Misri vs Ghana
  • Guinea vs Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Uchambuzi:Uganda vs Congo

Uganda Cranes ambayo kwa mara ya kwanza imefuzu kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwakani nchini Gabon, inatafuta nafasi nyingine ya kucheza katika kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

Uganda imejumuishwa katika kundi la E, pamoja na Misri, Ghana na Congo Brazaville.

Kundi hili linaogozwa na Misri kwa alama tatu, huku Ghana na Uganda zikiwa na alama 1. Congo Brazaville haina alama yeyote.

Mchuano wa kwanza, Uganda ikicheza ugenini mjini Tamale mwezi Oktoba, ililazimisha sare ya kutofungana katika mchuano huo muhimu.

Mara ya mwisho kwa nchi mbili kukutana katika mchuano wa kimataifa ilikuwa ni mwaka 2012 wakati wa michuano ya kufuzu kucheza fainali ya bara Afrika.

Mchuano wa kwanza, Uganda wakicheza nyumbani walipata ushindi wa mabao 4-0 lakni walipokwenda ugenini wakafungwa mabao 3-1.

Duniani, Uganda inaorodheswa ya 72 huku Congo ikiwa ya 55.

Kikosi cha Uganda:
Makipa: Denis Onyango (Mamelodi Sundowns Afrika Kusini), Odongkara Robert (St. George, Ethiopia), Jamal Salim (Al Merreikh, Sudan).

Mabeki: Denis Iguma, Godfrey Walusimbi (Gor Mahia, Kenya), Shafik Batambuze (Tusker FC, Kenya), Isinde Isaac, Jjuuko Murushid.

Kiungo wa Kati: Mukidi Ronald (Sweden), Mike Azira (Colorado Rapids, Marekani), Tony Mawejje, Geoffrey Kizito (Vietnam), Khalid Aucho (Baroka FC, Afrika Kusini), Yasser Mugerwa (St. George, Ethiopia), Moses Oloya (Urusi), Luwagga Kizito.

Washambuliaji: Yunus Sentamu (Finland), Miya Farouk (Standard Liege, Ubelgiji), Geoffrey Massa (Baroka FC, Afrika Kusini)

Kikosi cha Congo:
Makipa: Wolfrigon Mongodza (Diables-Noirs), Pavelh Ndzila (Etoile du Congo), Gildas Mouyabi (Lamancha).

Mabeki: Boris Moubhio, Carof Bakoua, Junior Epako, Gloire Yila Dibata (AC Leopards de Dolisie), Francis Okombi, Imouele Ngampio (JST), Dalvidy Ondzani (Etoile du Congo), Beranger Itoua (Cara), Saboukoulou (Patronage Sainte-Anne), Sagesse Babele (Diables Noirs), Guy Ndanga (JSP), Baudry Marvin (Zulte Waregem/ Begique), Arnold Bouka Moutou (Dijon/Ufransa), Christopher Samba (Panathinaikos/Ugiriki)

Viungo wa Kati: Dua Stanislas Ankira (AC Leopards de Dolisie), Duvald Ngoma (ASP), Kessel Tsiba Moukassa (Diables Noirs), Wilfrid Nkaya (JST), Alexandre Obambo (AS Cheminots), Giovanni Elvia Ipamy (Manga Sport/Gabon), Mervail Ndockyt (Tirana/Albania), Jordan Massengo (Union Saint Gilloise/ Belgium), Fabrice Nguessi Ondoma (Waydad Casablanca), Dzon Delarge (Osmanlispor/Turkey), Delvin Ndinga (Locomotive Moscow/Urusi), Prince Oniangue (Wolverhampton/Uingereza).

Washambuliaji: Guy Mbenza, Benny Boliko (JSP), Ismael Ankobo (ASK), Jacques Medina (La Djiri), Dore Ferebory (SCO Angers/ Ufaransa), Thievy Bifouma (Bastia/Ufaransa), Prince Vini Ibara (Club Bizertin/ Tunisia), Sylvere Ganvoula Mboussy (Waterloo/ Ubelgiji), Olongo Cedrick (Bng).

Uchambuzi wa DR Congo vs Guinea:

Leopard ya DRC inakwenda katika mchuano huu wa pili ikiwa inaongoza kundi la A kwa alama 3 sawa na Tunisia.

Mataifa mengine katika kundi hili ni pamoja na Guinea na Libya.

Mchuano huu unachezwa siku ya Jumapili katika uwanja wa Stade du 28 Septembre jijini Conakry.

Historia ya hivi karibuni kati ya nchi hizi mbili katika mechi tatu ilizocheza, kila nchi imeshinda mara moja kutoka sare mara moja na kupoteza mchezo mmoja.