TOUR OF RWANDA

Mashindano ya baiskeli ya Tour of Rwanda yashika kasi, yaingia steji ya 3

Sehemu ya waendesha baiskeli waliowahi kushiriki mashindano ya Tour of Rwanda.
Sehemu ya waendesha baiskeli waliowahi kushiriki mashindano ya Tour of Rwanda. http://www.tourdurwanda.rw

Mashindano ya baiskeli ya Tour of Rwanda, yemeshika kasi huku waendesha baiskeli wa Rwanda wakitoa ushindani mkubwa kwa washiriki wengine wa mwaka huu, ambapo Jumanne ya wiki hii walishika nafasi tatu za juu, katika hatua ya pili ya mbio hizo.

Matangazo ya kibiashara

Valens Ndayisenga, bingwa wa mbio hizo mwaka 2014 na sasa anaendesha baiskeli na timu ya Afrika Kusini ya Dimension Data for Qhubeka, ndiye aliyekuwa kinara wa siku kwa kushinda mbio za Kutoka Kigali na Karongi, zilizokuwa na umbali wa kilometa 124.7, akitumia muda wa saa tatu na dakika 16.

Ndayisenga alimshinda mpinzani wake wa karibu, Suleiman Kangagi anayeendesha na timu ya Kenya, akimshinda kwa alama moja.

Mshindi wa steji ya kwanza, Joseph Areruya ambaye anaendesha na timu ya Les Amis Sportif de Rwamagana, alimaliza katika nafasi ya tatu, akitumia muda wa saa 3 na dakika 18, dakika moja nyuma ya Ndayisenga.

Bingwa mtetezi wa mashindano hayo, Jean Bosco Nsengimana anayeshindana na timu ya Ujerumani Stradalli-Bike Aid, alimaliza katika nafasi ya tano akitumia muda wa saa 3 na dakika 18 sekunde 13.

Kufuatia ushindi wake, Ndayisenga alijinyakulia jezi ya njano ya uongozi wa mbio na pia kushinda zawadi ya mwendeshaji bora wa baiskeli kutoka Rwanda sambamba na ile zawadi ya Afrika.

Orodha ya Washindi wa jumla.

1. Valens Ndayisenga- Dimension Data 05h33’26”
2. Joseph Areruya- Les Amis Sportif 05h34’51”
3. Jean Bosco Nsengimana- Stradalli-Bike Aid 05h34’52”
4. Tesfom Okubamariam- Eriteria 05h34’58
5. Eyob Mitkel- Dimension Data 05h35’03”
6. Suleiman Kangangi-Kenyan Down Under 05h36’33”
7. Amanu Werkilul Ghebreigzabhier- Dimension Data 05h36’46”
8. MebraTemesgen Buru- Ethiopia 05h36’51”
9. Sebastien Fayard Fournet-Haute-Savoi/Rhone-Alpe 05h36’53”
10. Brett Wachtendorf- LowestRates 05h36’53”