FA

FA yawapiga marufuku wachezaji kutoka usiku wakiwa kwenye mechi za kimataifa

Wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza, wamezuiwa na chama cha soka cha nchi hiyo FA, kwenda kufanya starehe usiku wakati wakiwa kwenye michezo ya kimataifa.

Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Wayne Rooney
Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Wayne Rooney Reuters / Carl Recine Livepic
Matangazo ya kibiashara

Chama cha soka Uingereza FA, kimesema kuwa kinatazama madai kuwa wachezaji kadhaa wa timu ya taifa walienda kutembea usiku, baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Scotland, ambapo siku tatu baadae walikuwa na mchezo mwingine dhidi ya Uhispania, ambapo walitoka sare ya mabao 2-2.

Tayari nahodha wa timu hiyo ambaye pia ni nahidha wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney, ameomba radhi baada ya picha kumuonesha akiwa kwenye harusi moja usiku.

Katika hatua nyingine gazeti la The Sun limedai kuwa siku hiyo zaidi ya wachezaji 10 wa timu ya taifa ya Uingereza, walienda kwenye vilabu vya usiku na kunywa pombe hadi alfajiri ya kesho yake.

Katika taarifa iliyotolewa kwa niaba ya nahodha Wayne Rooney, ambaye usiku huo alihudhuria harusi kwenye heteli waliyokuwa wamefikia, imesema kuwa "Rooney anaomba radhi baada ya picha zilizopigwa na mashabiki kuchapishwa kwenye mtandao."

"Licha ya kuwa ilikuwa ni siku yao ya mapumziko pamoja na wakuu wa msafara, amekiri wazi kuwa picha zilizopigwa hazikuwa sahihi hasa kwa mtu muhimu kwenye timu kama yaye." alisema Rooney.

Uamuzi wa FA ambao haukutokana na kile kilichofanywa na Rooney pekee, haitegemewi pia kama FA itachukua hatua dhidi ya mtu yeyote.

Mkurugenzi mtendaji, Martin Glenn amesema kuwa "Msifanye maigizo kuhusu hili. Tunafanya uchunguzi unaostahili wa kilichotokea. Inasikitisha. Nikitendo kibaya na ameomba radhi. Alichokifanya hakioneshi mfano mwema kwa nahodha wa timu ya taifa, lakini sipendi kiongezwe chumvi."

"Je kulikuwa na maofisa wa FA waliohusika? Tunatafuta ukweli. Tunaongea na watu ambao walikuwepo kwenye tukio na kama waliwaona. Na vipi ufanye kitendo kama kile wakati unajua sheria kuhusu vilevi kwa wachezaji wa timu ya taifa zinajulikana? Lazima kuna maswali yataulizwa hakika.