Tour du Rwanda

Valens Ndayisenga ndio bingwa wa mashindano ya Tour du Rwanda 2016

Bingwa wa mashindano ya Tour du Rwanda 2016 Valens Ndayisenga
Bingwa wa mashindano ya Tour du Rwanda 2016 Valens Ndayisenga Faustin Niyigena

Valens Ndayisenga amekuwa Mnyarwanda wa tatu kushinda mashindano ya kila mwaka ya kukimbiza Baiskeli ya Tour du Rwanda.

Matangazo ya kibiashara

Mashindano hayo ya wiki moja yalimalizika mwishoni mwa wiki iliyopita katika uwanjwa Kimataifa wa Amahoro jijini Kigali baada ya wakimbiza baiskeli mbalimbali kutoka barani Afrika kumenyana kwa zaidi ya Kilimota 800.

Pamoja na kuwa mshindi wa mwaka huu, Ndayisenga ameweka rekodi ya kuwa mshindi mara mbili tangu mashindano haya, yalipoanza kuwavutia wakimbiza baiskeli wengine kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika mwaka 2009.

Licha ya Ndayisenga kumaliza katika nafasi ya tatu katika mzunguko wa mwisho, nyuma ya mshindi Tesfom Okubamariam kutoka Eritrea, bingwa huyo wa mwaka 2014 aliibuka bingwa wa mashindano hayo.

Alitawazwa bingwa baada ya kumalizika Kilomita 819.1 kwa muda wa saa 21, dakika 15 na sekunde 21.

Licha ya ushindi huo, mwenzake Eyob Metkel kutoka kampuni ya Dimension Data for Qhubeka ya Afrika Kusini alimaliza katika nafasi ya pili akiwa sekunde 39 nyuma kwa kutumia muda wa 21 na dakika 16.

Tesfom Okubamariam kutoka Eritrea alimaliza katika nafasi ya tatu katika mashindano ya mwaka huu.

Bingwa wa mwaka uliopita Jean-Bosco Nsengimana kutoka kampuni ya Ujerumani Stradalli Bike Aid, alimaliza katika nafasi ya 9.

Tano bora, Tour du Rwanda 2016
1.Valens Ndayisenga
2. Eyob Metkel
3. Tesfom Okubamariam
4. Joseph Areruya
5. Aman Werkilul Ghebreigzabhier